November 18, 2018


MPIRA UMEISHADAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89 Bado Tanzania inasukuma mashambulizi mengi yasiyo na macho
Dk 88 Tanzania wanaonekana kushambulia zaidi lakini bado mashambulizi yao hayana malengo
Dk 85, Lesotho wanaonekana kujilinda zaidi
SUB Dk 83 Abdallahkheri anatoka nje anaingia John Bocco
Dk 83, mchezaji mmoja wa Lesotho yuko chini baada ya kugongwa na Morris
Dk 80 Manula anafanya kazi nyingine ya kuokoa mpira ndani ya eneo la 18
Dk 77, Stars wanafanya shambulizi kali
Dk 76 GOOOOOOOOO mpira wa kona, Manula anaupangua, unapigwa kichwa na kujaa ndani
Dk 70 Lesotho wanafanya mabadiliko ya kuongeza washambulizi wawili, inaonyesha kocha anachotaka kujaribu mabao hatua ya mwisho
Dk 68 Toloane wa Lesotho anaachia mkwaju mkali nje ya eneo la 18, unatoka juu kidogo ya lango la Stars
Dk 64, Yondani anatolewa nje kutibiwa
Dk 63, Msuva anajaribu kumtoka beki lakini anamshitukia na kuokoa


Dk 61, mpira safi wa Msuva lakini pasi yake inakuwa ndefu
Dk 57 mpira wa adhabu wa Morris, kipa analazimika kufanya kazi ya ziada, kuokoa. Ilikuwa hatari sana
Dk 56, Msuva anawekwa chini nje kidogo ya 18
Dk 55, Stars wanaonekana kutawala wakishambulia mfululizo


Dk 52, mpira safi ulikuwa unakwenda wavunibaada ya kichwa cha Morris lakini beki anaokoa kwenye chaki
Dk 51, Chilunda anaruka vizuri na kupiga shuti, lakini kipa anaokoa na kuwa kona, inapigwa inaokolewa tena na kuwa kona tena
Dk 48, Kipa wa Lesotho anakaa chini, anaonyesha kama ana maumivu kwenye nyonga. Bado anatibiwa
Dk 46, Lesotho wameanza kwa kasi kubwa, wanapoteza nafasi nyingine kupitia Mafa katika mpira wa kona. Taifa Stars wanatakiwa kuwa makini




MAPUMZIKO
Dk 45, mpira wa krosi wa Taifa Srars lakini hakuna anayemalizia
Dk 43, Stars wanafanya shambulizi jingine lakini mambo yaleyale


Dk 40, Stars wanaonekana kufganya mashambulizi lakini si makali sana hasa wanapoingia eneo la lango
Dk 36, krosi safi kutoka kulia, Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa na Yondani anaokoa mpira uliokuwa unazama wavuni

D 29, Pasi ndefu ya Nyoni, lakini Msuva anachelewa na Lesotho wanaokoa

Dk 27, nafasi nyingine kwa Lesotho mpira wa kona lakini Manula anaokoa na kuwa kona nyingine
Dk 25, Lesotho sasa wanaonekana kutawala eneo la kiungo huku wakitengeneza mashambulizi zaidi

Dk 23, Kuthlang wa Lesotho anaonekana kuwa mwiba kwa beki ya Stars lakini shuti lake halikulenga lango
Dk 19, nafasi nyingine lakini shuti la Chilunda linakuwa nyanya kwa kipa wa Lesotho
Dk 14, nafasi nzuri kwa Lesotho lakini wanaokusosa mpira na Sonso anaokoa

Dk 8, Stars wanapoteza nafasi kupitia Chilunda.

Dk 2, Stars wameuanza mchezo kwa kasi kwa kutawala eneo la katikati.

3 COMMENTS:

  1. Kikosi kinabadilishwa badilishwa kila wakati, kweli kunahaja ya kuandaa wanajeshi tu

    ReplyDelete
  2. Yaan huyu kochaa sijui yukojee...mabeki gani wa pembeni aliwekaa

    ReplyDelete
  3. Kufungwa kumesababisababishwa na kocha. Kocha amependa sisi tufungwe. Kikosi gani kile alichokipanga. Anaanzisha wachezaji wa kati ambao hata kuwaona wakicheza nafasi hiyo kwa timu ya taifa hatujawahi kuwaona! halafu benchi anawaacha wachezaji wenye uwezo wa dimba la kati kama mkude, feisal! mbele hata alivyopanga mimi cjamuelewa! boko anamuachaje nje kwa dakika 92 zote wakati anajua mbwana samata hakuwa na nafasi ya kucheza! eti dakika ya 92 ndo anakuja kushituka kuanza kufanya sub, wakati sub ilitakiwa ifanyike hata kabla ya kwenda mapumziko, kwa maana udhaifu ulishaonekana upande wa beki, kiungo na ushambuliaji. Kiujumla jana kocha amefanya tustahili kufungwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic