Kikosi cha timu ya Taifa cha Tanzania 'Taifa Stars' leo kimeshindwa kuandika historia ya kukata tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kupoteza pointi tatu mbele ya Lesotho kwa kufungwa bao 1-0.
Stars wapo kundi L ambalo timu ya Uganda imefuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku timu ya Lesotho ikifikisha pointi 5 sawa na Stars, Cape Verde wana pointi 4.
Kwa kupoteza mchezo wa leo matumaini ya ya timu itakayoungana na Uganda Afcon Cameroni mwakani kwa kundi L yamebaki kwenye mechi za mwisho zitakazofanyika mwakani.
Stars watacheza na Uganda nyumbani mwezi Machi mchezo wa marudiano, huku Lesotho wakicheza na Cape Verde ambao wana pointi 4.
0 COMMENTS:
Post a Comment