November 18, 2018


Kikosi cha Namungo FC ambacho kinashiriki ligi daraja la kwanza kimeendeleza ubabe wake mbele ya vigogo wa soka Tanzania Yanga na Simba kwa kufanikiwa kutoa sare na timu zote mbili katika michezo ya kirafiki.

Yanga leo walikuwa wanacheza na Namungo FC katika uwanja wa Majaliwa, wamekubali sare ya kufungana bao 1-1.

Yanga walikuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza dakika ya 54 lililofungwa na Andrew Vincent huku Namungo wakisawazisha dakika ya 84 kupitia kwa Loriant Lusako.

Simba walicheza na Namungo Agosti 11 katika uwanja wa Majaliwa na kukubali sare ya kutofungana hali inayoonesha kwamba Namungo FC wameweza kupambana kibabe na vigogo hao wa soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic