November 20, 2018


Kocha Mbelgiji wa Simba, amesema hajawahi kuvutiwa na mchezaji yoyote Yanga hivyo hawezi kusajili yoyote ndnai ya timu hiyo. 

Patrick Aussems amesema wakati wa dirisha dogo la usajili hakutakuwa na chaguo lolote kutoka Yanga kama sehemu ya kuimarisha kikosi chake.

Mbelgiji huyo tayari inaelezw ameshaanda ripoti ya wachezaji takribani sita anaowahitaji ili kuisaidia timu kuelekea mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu kwa ujumla.

Moja ya majina yaliyotajwa ni kiungo mwenye ufundi mwingi kutoka Gor Mahia FC, Francis Kahata ambaye amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu.

Wakati huo Simba inaendelea kujifua kimazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi ujao dhidi ya Mwadui FC.

Simba inaendelea na tizi hilo bila ya uwepo wa beki wake wa kulia, Shomari Kapombe ambaye amepatwa na majeraha na hivi sasa yupo Afrika Kusini kwa vipimo.

1 COMMENTS:

  1. Uwe makini na post zako simba injiandaa dhidi ya Lipuri na sio mwafui . Mwadui alikubali kichapo cha 3-1 pale kambarage

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic