November 20, 2018


Na George Mganga

Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Harrison Mwakyembe, amesema matokeo ambayo Taifa Stars iliyapata juzi dhidi ya Lesotho kuelekea AFCON mwakani ndivyo mpira ulivyo.

Stars Jumapili ya wiki jana ilishuka dimbani kucheza na Lesotho kusaka tiketi ya kufuzu kwenda kucheza AFCON na ikakubali kupokea kichapo cha bao 1-0.

Mwakyembe ameeleza kuwa matokeo hayo ni sehemu ya mchezo hivyo hakuna tena namna zaidi ya kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Uganda.

Aidha, Mwakyembe amesema ataenda kumweleza Rais, John Pombe Magufuli kuwa wamefungwa kwa bahati mbaya lakini watajitahidi kupata matokeo dhidi ya Uganda kwenye mechi ijayo.

Waziri huyo mwenye dhamani ya michezo amefunguka kuwa atazungumza na Rais Magufuli ili kumuweka sawa baada ya kuwataka wachezaji wa Stars wakaje na ushindi huku akitoa milioni 50 za kuongeza hamasa.

Kuhusu fedha alizotoa Rais Magufuli, Makyembe amesema zimesaidia timu kutokufungwa mabao mengi kiasi cha kupelekea timu ipoteze kwa bao moja pekee.

5 COMMENTS:

  1. Ripoti ya hovyo na bahati nzuri Magufuli sio Mpumbavu anafahamu kuwa ni ripoti ya hovyo na si vizuri kujaribu kumpiga muheshimiwa raisi changa la macho mchana kweupe kwani maagizo ya amri jeshi mkuu hayakufuutwa matokeo yake tumepigwa na kajinchi kadogo tu. Kama Magufuli angelikuwa ndie mpeleka ripoti ya mechi kwa Nwakyembe kati ya Taifa Stars na Lethoso kamwe asingemumunya ukweli halisi ya nini kimetokea kule Maseru. Ni aibu tupu na kuidhalilisha nchi kimataifa. Burundi na vita vyao na hali isiyoeleweka kisiasa nchini mwao wanafanya vizuri na wananafasi kubwa zaidi ya kufuzu Afcon kuliko Tanzania. Hata Comoro kama si uwepo wa mshiriki muandaaji Cameroon katika kundi lao basi si lahasha komoro wangefuzu Afcon. Sasa sisi alieturoga nani? Tunapata Bahati ya dhahabu tunashindwa kuitumia halafu bado watu wanaleta siasa kwa kweli inakera. Hii hali ya kuchukulia poa watanzania kila tupofeli ndio chanzo cha kulea ufisadi kwani ni kufungua mianya kwa mafisadi kujua watanzania si watu wanaojali upotevu wa nguvu zao. Muheshimiwa raisi matarajio yake alijua mechi ile ya Lethoso hata tungeshindwa basi kila mtanzania angeridhika na vita kubwa itakayopigwa na vijana wetu lakini matokeo yake ni nyanya kabisa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kuongea upumbavu, mnaleta siasa kwenye mpira. Unawalaumu Stars kwa lipi? Nani asiyejua soka lilivyo? Unawanyooshea kidole, ni wapi Tanzania katika sekta zote imewahi kufanya vuzuri? Mafala kweli ninyi.

      Delete
  2. Siamini kwenye bahat mbaya..ila naamin kwenye makusudi. Piga chini wasaidiz wote waandamiz maana waneshindwa kumshaur vema. Haiwezekani msafara wenye watanzania lukuki alaf tumrshindwa kufanya maamuz sahihi. Haya bhana si yetu macho

    ReplyDelete
  3. Rais, toa amri, kocha hafai, uzembe wa kocha huuuuu, hiyo ripoti ya "mpira ndivyo ulivyo", ni ripoti ya majaribu tuu kwako mheshimiwa Rais. Kumbuka kodi ya watanzania imetumika pale, cha ajabu mtu anakuja kupanga kikosi kwa matakwa yake binafsi na chuki ambazo hazina maana! Au kocha anagombea wanawake na wachezaji? maana sio kwa chuki binafsi hizo. Arudi kwao huyu kocha, ameshatu-cost vya kutosha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic