November 20, 2018


Kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba 25 anasema anataka kuondoka Manchester United na kurejea Juventus. (Corriere dello Sport - in Italian)

Juventus wanajiandaa kumsaka raia wa England Marcus Rashford, 21, wakati wanaendelea kuonyesha nia ya kumsaini mshambuliaji huyo wa Manchester United. (Times - subscription needed)

Bisiktas wanasubiri mwezi Januari kumsaini mshambuliaji wa West Ham mwenye miaka 30 raia wa Mexico Javier Hernandez. (ESPN)

Arsenal pia wana mpango wa mwezi Januari kumwinda raia wa Uhispania Pablo Fornals, 22. Kiungo huyo wa kati wa Villarreal ana kipengee cha pauni milioni 17 cha kuvunja mkataba wake. (Sun)

Kiungo wa kati Mmarekani Christian Pulisic, 20, atahama Borussia Dortmund kujiunga na klabu ya Premier League lakini Chlsea na Liverpool wanasubiri msimu wa joto badala ya Januari. (Mirror)

AC Milan watatoa ofa kwa mchezaji wa chelesea na England mwenye miaka 32 Gary Cahill mwezi Januari. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud, 32, amesema hataondoka Chelsea akionya kuwa yuko tayari kupigania kikosi cha kwanza huko Stamford Bridge. (Mail)

Liverpool wanamlenga mfungaji bora wa Bundesliga Luka Jovic lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona na Bayern Munich kwa mshambualiaji huyo mwenye miaka 20 wa Frankfurt riawa Serbia.

Barcelona wamemtazama mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, na pia mshambuliaji wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23, akiwa naye mshambuliaji wa Frankfurt na Serbia Jovic msimu huu wakati wanamtafuta atakayechukua mahala pake mshambuliaji raia wa Uruguay Luis Suarez. (ESPN)

Barcelona wamempa ofa mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, ya kumtaka abadilishe mtindo wa maisha yake au aondoke klabuni. (Sport - in Spanish)

Uganda wafuzu kushiriki kombe la AFCON 2019
Wing'a wa Everton Ademola Lookman, 21, ametangaza utiifu wake kwa England kufuatia Nigeria kummezea mate. (Mail)

Uhispania na Ureno wanatafuta kufanya ofa ya pamoja na Morocco kuandaa kombe la dunia la mwaka 2030 kwa mujibu wa waziri mkuu wa Uhispania Sanchez said. (Reuters)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametupia mbali madai kuwa mlinzi raia wa Brazil Fabinho, 25, atahama klabu. (Liverpool Echo)

iungo wa kati wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, mchezaji wa zamani wa Newcastle anasema alivunjwa moyo wakati Steve McClaren alkifutwa kama meneja wa Newcastle United 2016. (Newcastle Chronicle)

Manchester United wametoa ofa ya pauni milioni 80 kwa mlinzi wakati wa Napoli raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (TyC via Manchester Evening News)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic