November 20, 2018


Kutokana na uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kuweza kuwavutia viongozi wa Simba kocha Mkuu kawagomea.

Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa hajavutiwa na mchezaji yoyote kutoka ndani ya Yanga hivyo Ajibu inabidi asubiri wakati mwingine kurudi Msimbazi.


"Hakuna mchezaji ambaye amenivutia kutoka ndani ya Yanga hivyo sina chaguo lolote la kumsajili mchezaji wa Yanga katika dirisha dogo kuimarisha kikosi," alisema.


Ajibu amekuwa na mwanzo mzuri kwenye ligi kwa kuwa amekuwa msaada ndani ya timu yake kwa kuhusika kutengeneza pasi 9 za mabao na kufunga mabao 3 kati ya 17 waliyofunga Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Kuna mtandao umesukwa kutokea Serikalini, Wizarani, Magazeti, waandishi wa Habari, BMT na TFF, Body ya Ligi na baadhi ya wanachama maarufu wa Yanga, kwa lengo la KUIHUJUMU NA KUIDHOOFISHA YANGA....mfano Uchaguzi angalia mchakato mzima....kabla, na wakati wa uchaguzi wenyewe. Angalia kwenye mechi ya kirafiki Namungo njoo kwenye wachezaji wa Timu za Taifa (u23 na Taifa Stars) hawajaripoti kambi ya Yanga kwenda kucheza mechi na mwadui...Bodi ya Ligi ingesogeza mechi yao ili kuruhusu wachezaji wao wajiunge na timu hawakufanya hivyo....ila Simba wameruhusiwa. Ukija kwenye mchakato wa ratiba za mechi zilizopangwa na bodi ya ligi....njoo uangalie sarakasi za uchaguzi...Swali Kwanini kakolanya, Yondani, ninja, kabwili na Paulo Godfrey hawatajiunga na Timu ili kuwahi mechi na Mwadui. Wenye akili tushajua hili...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanadai mshahara wao kaka. Walipeni wapige kazi. Acha kulialia bila sababu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic