November 20, 2018

Raisi wa nchi ya Uganda, Yoweri Museven amesema kuwa licha ya timu yake kufanikiwa kufuzu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) wanapaswa kushinda mchezo wao wa mwisho.

Uganda wamefanikiwa kufuzu baada ya kufikisha pointi 13 katika kundi L ambalo wapo pamoja na Tanzania ambayo ilipoteza nafasi hiyo baada ya kufungwa na Lesotho.


"Natambua kwamba mmefanikiwa kufuzu kushiriki Afcon na natambua kuwa mmebakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Tanzania, tafadhali hakikisheni mnashinda msipoteze," alisema.


Tanzania imejiweka kwenye mtego katika kundi L ili  kuweza kupenya kwenye hatua hii ni kuhakikisha wanaifunga Uganda na kusubiri matokeo ya Cape Verde kumfunga Lesotho ama kutoa sare.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic