November 18, 2018


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amewataja wachezaji wanne ambao ameitaka klabu ya Barcelona iwasajili kwenye dirisha la majira ya kiangazi.

Wachezaji hao ni Beki wa kulia wa Monaco, Djibril Sidibe, Mshambuliaji wa Genoa, Krzysztof Piatek, beki wa kati ya Ajax, Matthijs de Ligt na mmoja wapo kati ya Eden Hazard au Mohamed Salah kuchukua nafasi ya Ousmane Dembele.

Messi ameamua kuvunja ukimya kwa kuitaka Barcelona iwasajili wachezaji hao ili kukipa nguvu kikosi hicho ambacho kipo kwenye mashindano mengi ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Messi amemtaja Dembele kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa kuondoka muda wowote ule baada ya tetesi nyingi kuvuma dhidi ya Mfaransa huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic