November 24, 2018


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga , Mrisho Ngasa amesema kuwa anafurahia mafanikio anayoyapata ndani ya timu yake kwa kuwa yanatokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji pamoja na Mwalimu, Mwinyi Zahera.


Ngasa juzi aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa kwanza katika mechi yao ya nje ya Dar es Salaam  baada ya kucheza michezo 10 ndani ya Dar, kwa kufunga bao la ushindi akiwa nje ya 18 na likazama kwenye lango moja kwa moja.



 Ngasa alisema amekuwa katika wakati mzuri ndani ya Yanga na ataendelea kushirikiana na wachezaji wenzake kuweza kupata matokeo.

"Kitu kizuri ni kwamba tunashirikiana na wachezaji, tunacheza tukiwa ni timu hasa tukiwa uwanjani, hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa kazi bado inaendelea, mwalimu pia anatupa mbinu mbalimbali ambazo zinatusaidia kupata matokeo," alisema Ngasa.


Yanga wamefikisha pointi 29 baada ya kucheza michezo 11 wakiwa na mabao 19 mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic