November 24, 2018



 
Ofisa habari wa Singida United, Cales Katemana  amesema uongozi wa Simba umeamua kuwawekea ugumu kwa washambuliaji wao waliotaka kuwasajili kutokana na masharti yao.

Singida United wana mpango wa kusajili kwa mkopo wachezaji wawili kutoka Simba ambapo waliandika barua ili waweze kupata huduma ya wachezaji hao ila mpaka sasa bado mambo yamekuwa magumu.

"Uongozi wa Simba bado hatujafika nao muafaka mzuri kwa wachezaji wao ambao tulikuwa tunahitaji kuwachukua kwa mkopo, kama mipango itazidi kuwa migumu kwao 

tutatafuta wachezaji wengine," alisema.
  
Singida United tayari wamenasa saini ya mshambuliaji mwenye uraia pacha wa Norway na Liberia Dauda Bortu kwa mkataba wa miaka miwili wana mpango wa kupata washambuliaji wawili kutoka Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic