Kocha aliyeifunga timu ya Mbabane Swallows FC ya Swziland amewapa mbinu kali Simba ili kupata matokeo katika mchezo.
Iddy Cheche ambaye alikuwa kwenye benchi la ufundi mwaka 2017 wakati Azam FC wakiwanyoosha bao 1-0 Mbabane katika Uwanja wa Chamazi amesema kuwa Simba wana nafasi ya kushinda endapo watatumia vizuri uwanja wa nyumbani.
"Mbabane ni timu nzuri sio ya kubeza hasa wakiwa nyumbani wanatafuta matokeo kwa mbinu zote, ili Simba waweze kufanikiwa kupenya hatua ya mwanzo ni lazima wapate ushindi wakiwa nyumbani, tena washinde zaidi ya bao 1 kujiweka sehemu nzuri zaidi.
"Kushinda kwao wana fitina kutokana na figisu ambazo wanazifanya kwa sababu sisi kabla ya mechi tulifanyiwa vurugu, wachezaji na baadhi ya viongozi walipigwa, walitunyima uwanja wa kufanyia mazoezi makusudi, lengo lao kutotoa mchezoni walifanikiwa kwa kutufunga mabao 3-0 ," alisema.
Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems ambaye ni raia wa Ubelgiji na Mbabane wao wapo chini ya kocha Thabo Vilakati ambaye ni mzawa na anasifika kutumia staili ya 4-3-2-1.
Mbabane Swallows FC ya Swaziland watavaana na Simba kwenye mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika Novemba 28 Uwanja wa Taifa, Dar kisha Desemba 3 au 4 zitarudiana nchini Swaziland.
Asante cheche kwa ushauri mzuri kikubwa ni kwa wachezaji wenyewe kupambana sasa
ReplyDelete