November 13, 2018


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amesema kuwa anachotambua uchaguzi wa Yanga unafanyika Januari 1 mwakani na wa kujaza nafasi za viongozi waliojizulu.

Mwakyembe amesema klabu ya Yanga haiwezi ikaendeshwa bila ya kuwa na uongozi hivyo ni wakati mwafaka wa kufanyika kwa uchaguzi ili kujaza nafasi zote zilizo wazi.

Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo amekanusha taarifa zinazosema kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa amerejea kwenye nafasi yake akieleza ni taarifa za vijiweni na hawezi kuzingumzia.

Aidha, Mwakyembe amefunguka kuwa tayari wameshamaliza taratibu zote na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na akieleza mengine TFF watakuwa wanahusika kuyajibu.

"Tumeshamaliza taratbu zote na TFF, BMT na Yanga, hayo mengine yanayozungumzwa siwezi kuyasemea chochote mimi kwa maana si taarifa rasmi, ninachojua uchaguzi uko palepale kama ilivyopangwa" alisema Mwakyembe.

10 COMMENTS:

  1. TFF na Serikali kupitia Wizara na BMT na akina Mzee Akilimali (na wanaomtumia) msiivuruge amani ya nchi kwa kuchochea vurugu....Sauti ya Umma na Sauti ya Wengi ni sauti ya Moyo....kama Wanachama wa Yanga (Bara na Visiwani) wanampenda, na wamesema, na wameridhia, na Yeye amejibu kwa maandishi, na wamefuata taratibu na kanuni zote za katiba yao....Wasikilizeni kwani ndio hali halisi lazima ukubali, uchaguzi ufanyike kwa kujaza nafasi za M/Mwenyekiti, wajumbe 4....kufanya kinyume na hapa....ni kumkosea sio tu wananchi bara na Visiwani....(kwani historia na sura halisi ya klabu hii inaakisi umoja wa Kiafrika....kwani sio th ndio klabu kongwe na ya kwanza kuanzishwa wakati ule wa Tanganyika 1935 mwezi 2)....bali pia Mungu....(kwani ni sauti ya wanyonge)

    ReplyDelete
  2. Serikali (Wizara & BMT) na TFF, na Mzee Akilimali mnaweza mkasababisha damu kumwagika......ni tahadhari....kwani hoja ya msingi ni kwamba kwanini Simba haiingiliwa? Kwanini Serikali, BMT na TFF mmekuwa PARTIAL KATIKA SUALA LA UCHAGUZI HAMKUFANYA HIVYO KWENYE UCHAGUZI WA SIMBA....ILA WA YANGA MMEUINGILIA???...Mnajenga chuki. na kuleta uhasama kwa mioyo ya watanzania wanyonge wanaoupenda mpira wa miguu (Yanga ina waasisi wa uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar....na ndio maana Wanachama wake wako imara sehemu hizi 2 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)....mke wa Hayati Karume kule Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini la Young Africans Sports Club)...kwa hiyo kugusa na kuivuruga klabu kama hii...ni kuchochea kuvurugika kwa utulivu na amani ya nchi. Nchi ina mambo ya msingi ya kujikita nayo kuliko kuiingilia matatizo ya vilabu vya Yanga na Simba....waacheni waendelee kama wanasema Mwenyekiti wao bado yuko madarakani....kwenda kinyume na hili kunasababisha maswali kulikoni huko????

    ReplyDelete
  3. Endeleeni nawasubiri wapotee maboya Kama sijawapeleka FIFA,ngoja nivute subira.

    ReplyDelete
  4. Use your mind to think critically kwani barua ya manji inatakiwa isomwe na nani kuthibitisha kurejea kwake?msiwe mnaandika tu ilimradi,eti ataanza kazi rasmi tar15 January kwa maagizo ya daktari wake sawa ngoja tuone ila kaeni mkijua Mzee akilimali ana jicho pevu sana.anajua Janja Janja inayofanywa na yanga ili kuwatuliza mashabiki wake,but kiukweli kabisa hata kama manji amerudi si kwa matakwa yake mwenyewe.lengo ni kuhamasisha mashabiki na wachezaji wasipoteze morali na timu yao na ujanja huo ni wa kawaida sana huwa ni kawaida yao yanga kufanya hivyo,kama mtu alijiuzulu na bado mkasema yeye ni mwenyekiti wenu,pambaneni na hali yenu muacheni manji afanye mambo yake muda wake Wa kuingoza yanga umeshamalizika msimlazimishe,yanga ni timu kubwa kwann msitafute mbadala wa hilo jamani.

    ReplyDelete
  5. Ninavyojua mimi,TFF wameingilia suala LA uchaguzi yanga baada ya wao wenyewe yanga kusuasua na kama walishatoa mwongozo nakuainisha nafasi ambazo zipo wazi zijazwe na yanga kama club walilithibitisha hilo,hivyo kwa mabadiliko yoyote yale yanga inatakiwa ipeleke taarifa TFF ikiwa na vidhibiti haswaa lakini yanga hawajafanya hivyo,barua ya manji imesomwa na baraza la wadhamini likiongozwa na mkuchika ni sio TFF wala BMT pasi kuzingatia kwamba tayari suala hilo lilikua mikononi mwa serikali(TFF&BMT) baada ya yanga kusuasua,je hata kama ni wewe ungefanya nin hapo????kuweni wadadisi msiwe kama mashabiki maandazi bhana.

    ReplyDelete
  6. Ninavyojua mimi,TFF wameingilia suala LA uchaguzi yanga baada ya wao wenyewe yanga kusuasua na kama walishatoa mwongozo nakuainisha nafasi ambazo zipo wazi zijazwe na yanga kama club walilithibitisha hilo,hivyo kwa mabadiliko yoyote yale yanga inatakiwa ipeleke taarifa TFF ikiwa na vidhibiti haswaa lakini yanga hawajafanya hivyo,barua ya manji imesomwa na baraza la wadhamini likiongozwa na mkuchika ni sio TFF wala BMT pasi kuzingatia kwamba tayari suala hilo lilikua mikononi mwa serikali(TFF&BMT) baada ya yanga kusuasua,je hata kama ni wewe ungefanya nin hapo????kuweni wadadisi msiwe kama mashabiki maandazi bhana.

    ReplyDelete
  7. Use your mind to think critically kwani barua ya manji inatakiwa isomwe na nani kuthibitisha kurejea kwake?msiwe mnaandika tu ilimradi,eti ataanza kazi rasmi tar15 January kwa maagizo ya daktari wake sawa ngoja tuone ila kaeni mkijua Mzee akilimali ana jicho pevu sana.anajua Janja Janja inayofanywa na yanga ili kuwatuliza mashabiki wake,but kiukweli kabisa hata kama manji amerudi si kwa matakwa yake mwenyewe.lengo ni kuhamasisha mashabiki na wachezaji wasipoteze morali na timu yao na ujanja huo ni wa kawaida sana huwa ni kawaida yao yanga kufanya hivyo,kama mtu alijiuzulu na bado mkasema yeye ni mwenyekiti wenu,pambaneni na hali yenu muacheni manji afanye mambo yake muda wake Wa kuingoza yanga umeshamalizika msimlazimishe,yanga ni timu kubwa kwann msitafute mbadala wa hilo jamani.

    ReplyDelete
  8. Dude, hivi bila manji yanga haiwezi kwenda au, mnamng'ang'nia mtu hana utayari, huo nao niudhaifu nakutojiamin

    ReplyDelete
  9. Nnachoona hapa ni kwamba yanga wanamlilia Manji kwa Vile Mo Yuko simba.kama mnataka badilisheni mfumo was uendeshaji mo awe mwekezaji.kwani akiwa mwenyekiti atakuwa na sauti kuliko wanachama na pia atataka kukodisha timu kama kama viti vya kwenye harusi

    ReplyDelete
  10. Yanga walishabadilisha mfumo wa uendeshaji wa Club tangu 2006 ila serikali wakati huo wakaona Yanga watafaidi sana wakachochea migogoro ndiyo zikatokea Yanga Asili na Kampuni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic