November 21, 2018


Kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu ya Yanga Januari 1 2018, Mwanachama Lusajo Kisanda kutoka Nyanda za Juu Kusini ameibuka na kupongeza harakati za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa namna ilivyochangia mchakato kwend kasi.

Kisanda ameeleza kuwa TFF ilisaidia mpaka mchakato wa kuweza kushika kasi ambapo mpaka sasa zoezi la uchukuaji wa fomu limeshakamilika.

Amesema kinachotakiwa kwa sasa ndani ya klabu ni kuhakikisha uchaguzi unakuja kufanyika salama na hakuna haja ya kuleta malumbano ambayo hayana msingizi.

Mwanachama huyo amefunguka kuwa hakuna namna Yanga kuendelea kuongozwa bila ya viongozi hivyo inabidi uchaguzi ufanyike ili kujaza nafasi za viongozi ambao hawapo madarakani.

Aidha,ameongeza kuwa ni wakati mwafaka wa wanachama wa klabu kufanya maamuzi sahihi ili kumpata Mwenyekiti wa klabu baada ya kutokuwa naye kwa takribani mwaka mmoja na nusu sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic