November 20, 2018


Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 23, Bakari Shime amesema kuwa kilichosababisha waweze kufungwa bao dakika za lala salama ni presha ya wachezaji ndani ya uwanja.

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 ilikuwa kibaruani leo ikicheza na timu ya Taifa ya Burundi mchezo wa marudiano wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya ule wa awali uliochezwa Burundi kupoteza kwa kufungwa bao 2-0.


"Baada ya wachezaji kupata matokeo ya bao 3 presha kubwa ikwa kwenye kulinda bao, hali iliyofanya washindwe kuwa makini na kosa moja walilofanya wakaruhusu bao dakika za lala salama, hakuna namna tumejifunza," alisema.


Kwa matokeo hayo timu ya Taifa imetolewa kwenye michuano hiyo kwa faida ya bao la ugenini ambalo Burundi walilipata dakika ya 89.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic