Timu ya Namungo FC imepania kuwavuruga wapinzani wao Yanga katika mchezo wao wa kirafiki utakaochezwa November 18 katika Uwanja Majaliwa, uliopo Mtwara.
Namungo FC, inashiriki ligi daraja la kwanza imepania kuhakikisha inavunja rekodi ya Yanga kutopoteza katika michezo yake ya kirafiki ambayo wamecheza hivi karibuni pamoja na ile ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ofisa habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa wanatambua kwamba Yanga ni timu kubwa na inawachezaji wenye uwezo ila wao watawaonyesha kwamba wamedhamiria kuweka rekodi kwa vigogo hao wa ligi.
"Tumejipanga kuhakikisha tunaweka rekodi ya kipekee kwa kuwafunga mabao ya kideoni na tumejiandaa kuonyesha mpira wa darasani, hivyo tutaushangaza ulimwengu wa mpira, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona maajabu," alisema.
Namungo waliwahi kucheza na Simba katika mchezo wa kirafiki na kulazimisha sare ya kutofungana, hivyo watakuwa na kazi ya kucheza na vigogo Yanga ambao wametoka kumfunga African Lyon katika mchezo wao wa kirafiki uliochezwa jana Uwanja wa Uhuru.








TFF na Serikali kupitia Wizara na BMT na akina Mzee Akilimali (na wanaomtumia) msiivuruge amani ya nchi kwa kuchochea vurugu....Sauti ya Umma na Sauti ya Wengi ni sauti ya Moyo....kama Wanachama wa Yanga (Bara na Visiwani) wanampenda, na wamesema, na wameridhia, na Yeye amejibu kwa maandishi, na wamefuata taratibu na kanuni zote za katiba yao....Wasikilizeni kwani ndio hali halisi lazima ukubali, uchaguzi ufanyike kwa kujaza nafasi za M/Mwenyekiti, wajumbe 4....kufanya kinyume na hapa....ni kumkosea sio tu wananchi bara na Visiwani....(kwani historia na sura halisi ya klabu hii inaakisi umoja wa Kiafrika....kwani sio th ndio klabu kongwe na ya kwanza kuanzishwa wakati ule wa Tanganyika 1935 mwezi 2)....bali pia Mungu....(kwani ni sauti ya wanyonge)
ReplyDeleteSerikali (Wizara & BMT) na TFF, na Mzee Akilimali mnaweza mkasababisha damu kumwagika......ni tahadhari....kwani hoja ya msingi ni kwamba kwanini Simba haiingiliwa? Kwanini Serikali, BMT na TFF mmekuwa PARTIAL KATIKA SUALA LA UCHAGUZI HAMKUFANYA HIVYO KWENYE UCHAGUZI WA SIMBA....ILA WA YANGA MMEUINGILIA???...Mnajenga chuki. na kuleta uhasama kwa mioyo ya watanzania wanyonge wanaoupenda mpira wa miguu (Yanga ina waasisi wa uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar....na ndio maana Wanachama wake wako imara sehemu hizi 2 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)....mke wa Hayati Karume kule Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wadhamini la Young Africans Sports Club)...kwa hiyo kugusa na kuivuruga klabu kama hii...ni kuchochea kuvurugika kwa utulivu na amani ya nchi. Nchi ina mambo ya msingi ya kujikita nayo kuliko kuiingilia matatizo ya vilabu vya Yanga na Simba....waacheni waendelee kama wanasema Mwenyekiti wao bado yuko madarakani....kwenda kinyume na hili kunasababisha maswali kulikoni huko????
ReplyDelete