Kampuni ya kutengeneza vifaa ya Nike, imetengeneza jezi maalum ya FC Barcelona kusherekea miaka 20 ya kufanya kazi na klabu hiyo.
Nike imetengeneza jezi hiyo ikiwa na aina zote za mitindo ya jezi ya Barcelona iliyobadilika kwa misimu tofauti ndani ya miaka 20.
Jezi hiyo inaonyesha rangi zilezile lakini katika mitindo tofauti iliyobuniwa na Nike kwa ajili ya Barcelona, klabu kubwa kati ya mbili za Hispania. Nyingine ni Real Madrid.
Barcelona na Madrid ni kati ya klabu maarufu zaidi tano duniani kote katika mchezo wa soka licha ya kwamba zinamiliki timu za michezo mingine kama ule wa kikapu.
0 COMMENTS:
Post a Comment