November 12, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Obrey Chirwa ameanza rasmi mazoezi na timu yake mpya leo katika uwanja wa Chamanzi ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

Chirwa ambaye ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Novemba 15, akiwa amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ni pendekezo la benchi la ufundi linaloongozwa na Hans Pluijm.

Meneja wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa mipango yao ni kuweza kuona wanafanikiwa kufikia malengo yao hasa kwa kuweza kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani.

"Tuna wachezaji wazuri ambao wana juhudi na hicho ndicho kinachotupa raha kwa kuwa kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo, wakati ni sasa kuhakikisha tunaweza kuwa na kikosi bora," alisema.

Chirwa anaungana na mchezaji mwenzake wa Zamani ambaye alikuwa anacheza naye timu ya Yanga, Donald Ngoma na wote ni raia wa Zambia kuitumikia timu ya Azam FC.

2 COMMENTS:

  1. Duh! Ngoma ni raia wa zambia? mara ya pili hii nakuona unarudia kusema ngoma ni raia wa zambia andikeni habari kwa weledi basi acheni mihemko

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic