November 2, 2018


Neema imeendelea kuwashukia wachezaji wa Simba, unaambiwa kama mchezaji akicheza mechi ya Ligi Kuu Bara na timu ikapata ushindi, basi anapata posho ya shilingi 400, 000.

Kiasi hicho cha fedha kinapita baadhi ya waajiriwa wa Serikalini wakiwemo walimu na manesi ambao mishahara yao ya kila mwezi inakadiriwa kuanzia shilingi 300, 000.

Ukikusanya posho za mechi moja za Okwi na Claytous Chama zinaweza kulipa mshahara wa beki chipukizi wa Yanga, Paulo Godfrey ambaye juzi kwenye mechi dhidi ya Lipuli alilimwa kadi nyekundu. Simba hadi hivi tayari imecheza michezo kumi ya ligi huku ikashinda mechi saba, ikafungwa mchezo mmoja na Mbao FC na sare mbili dhidi ya watani wao Yanga, Ndanda FC.

Taarifa ambazo tumezipata ni kwamba, posho hizo za 400,000 zinawahusu wale wachezaji wanaocheza mechi pekee na wanaokaa jukwaani wanaambulia uchakavu wa shilingi 80,000 pekee katika mchezo.

Mmoja wa vigogo wa Simba alisema wameweka kiwango hicho fedha kwa ajili ya kuongeza ushindani wa wachezaji ndani ya uwanja ili mmoja akipata nafasi ya kucheza, basi acheze kwa kiwango cha juu kwa mafanikio ya timu.

Alipotafutwa Mratibu wa timu hiyo kuzungumzia hilo, Abbas Ally alisema: “Posho kwa wachezaji zipo katika kuhakikisha morali ya wachezaji inaoongezeka ambayo ni siri nisingeweza kuiweka wazi.”.

CHANZO: SPOTI XTRA

3 COMMENTS:

  1. Acha projo zako, nani kakuambia mshahara w Mwalimu 400,000/= au Nesi 300,000? Fanya utafiti kwanza kabla ya kukurupuka!

    ReplyDelete
  2. Acha ukorofi wako Wa ulinganifu Wa posho na mishahara ya wachezaji vikabuni.Hizo ni fitina na chengachenga za hila.Wachezaji wrote wanajua kuwa IPO tofauti ya posho na mishaha..hats ndani ya simba wachezaji hutofautiana mishahara.Wachezaji wrote wanajua hill.huko Ulaya nako ni vivyohivyo.were ni mfitanishi tu.Kwa mini usizungumzie Costal union na simba hiyo tofauti unayo Iona.watu mtk timu hao hawaangalii hayo,,watu hutafuta ubingwa,magoli na makombe yaliyoingizwa na wachezaji haohao wanaopokea Lima cha chini.

    ReplyDelete
  3. Binafsi nakubaliana na wachezaji kutofautiana mishahara , lakini katika suala la posho siliafiki. kwani timu imesajiri wachezaji 30 , lakini wanaotakiwa kucheza na benchi la akiba ni 18 tu . Hivyo kinyang'anyiro cha namba na kufukuzia posho kinawabagua na huenda umoja ndani ya wachezaji ukapungua na kunaweza kusababisha kuumizana mazoezini kwa kupigania namba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic