November 2, 2018






Na Mwandishi Wetu       
Uongozi wa Yanga umesema kuwa bado unatambua Yusuf Manji bado mwenyekiti wao hadi pale watakapopokea barua kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya maagizo ya kuitisha uchaguzi.

BMT juzi iliitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizuru huku ikiwemo ya mwenyekiti wao Yusuf Manji aliyeiandika barua ya kujiuzuru hivi karibuni.

Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe sita kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten alisema wao hawawezi kulizungumzia hilo hadi watakapopata barua kutoka BMT na TFF.

Ten alisema, hawana taarifa ya kiofisi waliyoipata kutoka BMT na TFF juu ya agizo hilo huku ukiahidi kulifanyia kazi hilo baada ya kupokea barua kutoka kwenye chama na shirikisho hilo la soka.

“Nisingependa kulizungumzia hilo la uchaguzi hivi sasa, niwe mkweli kama Yanga hatukupata barua la kiofisi kutoka BMT na TFF ya kutuagiza kufanya uchaguzi wa baadhi ya wajumbe wa timu na mwenyekiti wetu.

“Hivyo, nitalizungumza hilo baada ya kupokea barua kutoka BMT na TFF, hivyo nitakavyoweza kusema kwa hivi sasa,’alisema Ten

3 COMMENTS:

  1. Hizi vuta nikuvute zinawarudisha nyuma Yanga. Mnasubiri barua halafu mkae kikao tena halafu tarehe itangazwe mtakuwa mmechelewa....Ilitakiwa mfanye uchaguzi haraka tena ikiwezekana tarehe 24 mwezi wa 11. Kwanini Simba wao mambo yao hayakwami katiba mpya imepita uchaguzi unafanyika...making huku Yanga ni vuta nikuvute na malumbano pamoja na mabishano na hivi kuna nini huko? Fanyeni uchaguzi ili muendelee na ligi na usajili msijicheleweshe....Kuna watu wanataka mvurugane na kujichelewesha ili Simba ifanikiwe kuweni makini kwa kuyaepuka hai!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizi vuta nikuvute zinawarudisha nyuma Yanga. Mnasubiri barua halafu mkae kikao tena halafu tarehe itangazwe mtakuwa mmechelewa....Ilitakiwa mfanye uchaguzi haraka tena ikiwezekana tarehe 24 mwezi wa 11. Kwanini Simba wao mambo yao hayakwami katiba mpya imepita uchaguzi unafanyika...lakini huku Yanga ni vuta nikuvute na malumbano pamoja na mabishano na hivi kuna nini huko? Fanyeni uchaguzi ili muendelee na ligi na usajili msijicheleweshe....Kuna watu wanataka mvurugane na kujichelewesha ili Simba ifanikiwe kuweni makini kwa kuyaepuka hayo

      Delete
  2. Barua imetumwa kwa e-mail kutoka BMT na nakala kupelekwa Yanga, TFF na Wizarani na hata baadhi ya vyombo vya habari viliipokea na kuichapisha hadharani sasa mnasubiri barua ipi? Kama sio jitihada za kujichelewesha tu ili muendelee katika hali iliyopo ambayo si yenye kuleta tija na maendeleo katika uongozi wa mpira. Klabu haiwezi kukaa bila ya Uongozi...kwa muda wote huu. Inatakiwa inapoanza mwezi 12 tayari muwe na uongozi!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic