November 14, 2018







Kocha Salvisa Jokonovic wa Fulham anakuwa wa kwanza kutimuliwa msimu huu na nafasi yake inachukuliwa na kocha wa zamani wa Leicester City, Claudio Ranieri.

Ranieri aliyewahi kuinoa Chelsea, alifanikiwa kubeba ubingwa wa England misimu miwili iliyopita akiwa na Leicester na kuushangaza ulimwengu wa soka.

Baada ya mechi 12 chini yake, Fulham iliyofanya usajili wa kukata na shoka, imekusanja pointi tano pekee.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Fulham umeamua kumuondoa mapema ili kuhakikisha wanajiimarisha mapema na kujiondoa katika hatari ya kuteremka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic