DK TIBOROHA |
Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Dk Tiboroha amechukua fomu kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Yanga.
Taarifa za Dk Tiboroha ambaye alikuwa katibu mkuu chini ya uenyekiti wa Manji, zimejulikana leo katika makao makuu ya klabu hiyo.
Pamoja na Dk Tiboroha ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mwingine aliyechukua fomu ya kuwania mwenyekiti ni Yono Kevela.
Kevela ambaye ni mmiliki wa Yono Auction Mart, kampuni maarufu ya minada ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Njombe.
Pamoja na hao, Tito Osora naye amejitosa kwa ajili ya uchaguzi huo utakaofanyika mapema mwakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment