November 20, 2018


Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa kesho Jumatano 21/11/2018 umesogezwa mbele na sasa utachezwa siku ya Ijumaa 23/11/2018.

Mabadiliko hayo yamefanywa ili kuwapa nafasi wachezaji wetu waliokuwa kwenye timu zao za Taifa kujiunga na kikosi chetu ili kuwa sehemu ya wachezaji ambao watacheza mchezo huo.

Ukaichana na wachezaji hao, Simba itamkosa beki wake wa kulia Shomari kapombe ambaye ameumia akiwa kambini na timu ya taifa 'Taifa Stars'.

Tayari Kapombe ameshaanza kufanyiwa matibabu huko Afrika Kusini ili kurejea katika hali yake ya kawaida hapo baadaye.

10 COMMENTS:

  1. Kuna mtandao umesukwa kutokea Serikalini, Wizarani, Magazeti, waandishi wa Habari, BMT na TFF, Body ya Ligi na baadhi ya wanachama maarufu wa Yanga, kwa lengo la KUIHUJUMU NA KUIDHOOFISHA YANGA....mfano Uchaguzi angalia mchakato mzima....kabla, na wakati wa uchaguzi wenyewe. Angalia kwenye mechi ya kirafiki Namungo njoo kwenye wachezaji wa Timu za Taifa (u23 na Taifa Stars) hawajaripoti kambi ya Yanga kwenda kucheza mechi na mwadui...Bodi ya Ligi ingesogeza mechi yao ili kuruhusu wachezaji wao wajiunge na timu hawakufanya hivyo....ila Simba wameruhusiwa. Ukija kwenye mchakato wa ratiba za mechi zilizopangwa na bodi ya ligi....njoo uangalie sarakasi za uchaguzi...Swali Kwanini kakolanya, Yondani, ninja, kabwili na Paulo Godfrey hawatajiunga na Timu ili kuwahi mechi na Mwadui. Wenye akili tushajua hili...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumia akili, simba ina wachezaji kama kagere, okw, juuko, chama hawa wana safari ndefu kufika Tz, Tumia akili wewe gendaheka sio kulaumu tu.

      Delete
    2. Mna kikosi kipana vipi mtegemee hao tu ......ww akili yako pumba tu kisa wachezaji hao ndio mechi isogezwe mbele ?

      Delete
  2. Hiyo ndiyo Mbereko fc walijinasibu kuwa wanakikosi kipana leo wanaomba poo kwa Lipuli haahaaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mfa maji hakosi kutapatapa pole kwa kuanza mapema

      Delete
  3. Endeleen kubebana ila laana inaangukia timu ya taifa kisa yanga mnakoxa uxingiz?

    ReplyDelete
  4. Jamani wadau wenzangu chama la wananchi (yanga) , tupambaneni na hali yetu hao wenzetu kwa sasa ni matawi ya wanaweza kufanya lolote na kwa wakati wowote

    ReplyDelete
  5. Kichwa cha habari kinaonyesha namna gani ulivyo mbumbumbu na huna akili na unachofikiria were ni Simba.Kwani wachezazi wa Yanga wanaocheza timu ya taifa watakuwa hawajarudi?Au Yanga watacheza kabla ya wachezaji hao kuwasili?Au simba inacheza mechi baada ya Yanga kuwa imecheza katika Siku tofauti?Wachezaji kama Yondani na Kakolanya hawatachezea Yanga kwa kuwa wamegoma.We we mwandishi ni kichwa maji kweli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic