November 19, 2018


 

Kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati ya uchaguzi ya TFF iliyo chini ya Mwenyekiti Malangwe Mchungahela kutoa agizo la kufanyika uchaguzi kwa nafasi zote ndani ya Yanga, Januari 13 mwakani uongozi umetoa msimamo kwa wanachama.

Kamati ya uchaguzi imeagiza kufanyika kwa uchaguzi kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti ambaye baraza la wadhamini walisoma barua kurejea kwa Yusuf Manji hali ambayo inawafanya waamini kwamba mwenyekiti yupo isipokuwa makamu na nafasi nyingine ndio zitajazwa.


 Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Hussen Nyika amesema kuwa wanachama wanapaswa watulie hasa katika kipindi hiki cha mpito kwa kuwa uongozi unasimamia katiba.

"Hatuwezi kuisigina katiba kwa kuwa tunaitambua na tunaendesha kazi kwa kufuata miongozo hivyo wanachama wanapaswa watulie ili tuweze kusimamia haki, sisi tunatambua kwamba Mwenyekiti wetu ni Manji bado yupo hivyo hatuwezi kukubali kuyumbishwa.


"Kikubwa tunachokifanya kwa sasa ni kufuata katiba, tunajua kwamba kuna nafasi ambazo zipo wazi hilo kwetu halitupi shida tutafanya uchaguzi ila kwa nafasi ya Mwenyekiti itabaki kwa kuwa ina mtu, " alisema Nyika.

2 COMMENTS:

  1. Shauri yenu, mnatafuta makubwa nyinyi, na bora hamna uwakilishi kimataifa, kwa sababu mngetuponza kama alivyotuponza AMUNIKE. Kwasasa naona mnawatafuta FIFA kuwafungia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni simbaba mfunga tai nyekundu Hamu yenu ni kuona Yanga inasambaratika.Hatuingii kwenye mtego wako.ngoo!! Uwe umetumwa au ni kwa maslai yako binafsi siingii mtego wako ngooo.Maji bado ni mwenyekiti wetu.Yanga ni chama cha watu kinakatiba yake,Amulike ni binge LA Kocha usimlinganishe na mzungu wenu semale hakumpnga Mkude,

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic