November 20, 2018


Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema kuwa watanzania waache kumsemea Rais John Magufuli kuhusu milioni 50 alizotoa kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema kuwa wameumia kwa kupoteza mchezo wao dhidi ya Lesotho ila wanaamini kwamba Stars itafuzu michuano hiyo kwa kuweza kushinda nyumbani na kuwataka wanaozungumzia masuala ya pesa za Rais Magufuli waache.


"Wanaozungumzia pesa alizotoa Rais waache kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wanamsemea wakati yeye hajasema hivyo watulie, Rais anajua mpira na anafuatilia pia hivyo waache kufanya hivyo.


"Nina matumaini ya kuweza kufuzu kwa timu yetu hasa kutokana na uwezo wa kupata matokeo tukiwa nyumbani kama ambavyo tulifanya dhidi ya Cape Verde ndivyo tutakavyofanya dhidi ya Uganda," alisema.


Rais Magufuli alitoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya maandalizi ya Stars kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Lesotho ambao wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0 na aliwaagiza kuja na ushindi wakishindwa alisema watazitapika.

8 COMMENTS:

  1. hizo pesa alizotoa Magufuli ni kodi zetu kwa hiyo lazima tuzisemee wewe una mamlaka ya kutuambia tunyamaze

    ReplyDelete
  2. Rais wetu wa TFF, huwezi kuwaziba mdomo watanzania, kila mmoja ana uchungu wa aina yake, safari hii Stars haikuwa na sababu yoyote ya kushindwa kuwafunga Lesotho kwao. Kwamaana maandalizi ndiyo ambayo huwa kisingizio kikubwa kwa mechi nyingi za Timu ya Taifa, lakini safari mmepewa fedha ambazo hata hamkuzitarajia. na pia mmepewa na mtu ambaye hata hamkutarajia atatoa fedha. Mnapata wapi sababu ya kusema kuwa watanzania tusiseme? na kwanini tusiseme? Pia, jambo lingine labda hukumuelewa Rais, alisema kuwa zile fedha ni za walipa kodi, mkifungwa na Lesotho, tafuteni cha kuwaambia walipa kodi. Sasa hiki ndicho mnachotuambia baada ya kufungwa na Lesotho? Ilikuwa ni busara kwa kipindi hiki kuwaacha watanzania wamalize hasira zao zote kulingana na hisia zao na maumivu waliyoumizwa nayo kutokana na matokeo mabaya ya kujitakia, baada ya hapo mlitakiwa mje na kauli yenu iliyojaa misamaha mingiiiiiii, na pia mlitakiwa mje na solution, na sio kuanza kushindana na watanzania kwa kile walichokiona kwamba wamefungwa kwasababu ya UTASHI wa watu wachache au mtu mmoja tu. Hii inashangaza sana, na inaweza ikawa ipo Tanzania tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani hawa TFF maboga kabisa sijui huyu kocha walimpata kwa vigezo vipi?

      Delete
  3. Replies
    1. Rais wa TTF usitunyamazishe watanzania, kiufundi tff inaonekana ni wababaishaiji. mnateua technical benches sijui kwa creteria zipi???? amunike hatufai, Ninje hatufai na mkurugenzi wa ufundi hatufai sidhani kama kuna maendeleo ya kisoka hapo. Karia jitathimini leo pia tumetolewa na Burundi. Afadhali ya TFF ya Malinzi na siyo hii.

      Delete
  4. Enter your comment...Kocha wetu inaonekana hatunzi kumbukumbu hajui mechi ya kwanza ya capvede alipotezaje na Pili alishindaje. Angekuwa na kumbukumbu tusingefungwa na lethoso. Siamini kwa mini tulifungwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic