November 13, 2018


 
Baada ya kucheza michezo 10 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, uongozi wa Yanga umebuni mbinu itakayowafanya waweze kuwa sawa katika michezo yao ya nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza kucheza michezo ya kirafiki ambapo walianza na African Lyon kesho watacheza na Reha Uwanja wa Uhuru.

 Kaimu katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaya amesema kuwa lengo kubwa la kucheza michezo hiyo ni kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zao za ligi ambazo wataanza kutoka nje ya mkoa wa Dar.

"Tunacheza michezo ya kirafiki ili kuweza kujiweka tayari kuwakabili wapinzani wetu Mwadui FC katika mchezo wetu wa ligi kuu ambao tutatoka nje ya Dar," alisema.
 
Yanga watacheza na Mwadui FC ya Shinyanga November 22, Shinyanga ikiwa ni mechi yao ya kwanza nje ya Dar msimu huu, Novemba 17 watasafiri kwenda mkoani Mtwara kwa ajili ya kucheza na Namungo FC mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Majaliwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic