November 23, 2018


Baada ya Simba kupata sare ya kutofungana na timu ya Lipuli FC, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Taifa, uongozi umefunguka mipango yao ijayo.

Simba wametoka sare mchezo wao wa 3 wakiwa wameshinda michezo 8 na kupoteza mchezo mmoja kati ya 12 waliyocheza.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema hayo ni matokeo ya mpira hivyo akili zao ni kwenye maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa wa Ligi Kuu ya Mabingwa Afrika.

"Huu ni mpira na haya ni matokeo, hivyo hakuna namna. sasa nguvu zetu tunazielekeza katika mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows FC ya kutoka Swaziland, utakaochezwa jumatano," alisema.

Matokeo hayo yanawafanya wavune pointi moja uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya pointi 27 wakiachwa na Yanga ambao jana walishinda mbele ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga na kufikisha pointi 29.

8 COMMENTS:

  1. Kwa uchezaji aliocheza Mkude leo wakati mwingine unawaza may be Amunike is right,mwisho wa siku unaona kuwa kama Taifa mpira bado.

    ReplyDelete
  2. Leo unasema hayo ..kwenda huko na madharau yako.

    ReplyDelete
  3. Kwani Mkude alicheza peke yake kwenye timu? Naona bado wadau wanahangaika kumsafisha Amunike na utumbo alioufanya kule maseru Lethoso. Taifa stars kama wangepata matokeo walioyoyapata Simba ya kutoka sare basi ingekuwa poa tu kwani simba haikufungwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Taifa Stars ingepata sare ingekuwa poa ya nini wakati bado ingekuwa lazima kutakiwa kushinda mechi ya mwisho

      Delete
  4. Dah namna hii kukosa magoli mengi kiasi hiki, timu isipobadilika basi kuna droo au kufungwa na Mbabane u/Taifa, kisha kupoteza kwa goli za kutosha huko ugenini. Kocha anapaswa afanye kazi kubwa sana has a kwa fowadi ili kuongeza sana umakini wa eneo la umaliziaji. Hapa pia ndipo kunapoonekana umuhimu wa kusajili beki 1 wa kulia pamoja na forward 1 wa Kariba ya OKWI. Coach hakwepi kusajili fowadi hapa vinginevyo siamini km kuna kutetea ubingwa.

    ReplyDelete
  5. Simba kutoka sare na Lipuli kama mdau wa simba ninaeipenda Simba hadi kufikia kuomba day off nipate wasaa mzuri wa kuifuatilia timu yangu licha yakwamba kukosekana kwangu kazini siku moja huwa ninaacha mzigo mkubwa mahala pangu kwa kazi na kunanikosesha kiasi cha maana cha fedha na hata wakuu wangu wa kazi hawanielewi kwa hivyo nikiri matokeo ya aina hii tuliyoyapata kwa lipuli yananiumiza sana lakini ndio mpira. Kutoka mechi na kagera sugar ya kukabidhiwa kombe mbele ya muheshimiwa raisi ilikuwa ni aibu. Na siwezi kusema Mfaransa yule hakuwa kocha hata Simba ifungwe mbele ya muheshimiwa raisi na kitimu cha kawaida tu. Na sithubutu kusema huyu Mbeligiji si kocha kamwe sitasema hivyo kwani niliishuhudia leopard ya Congo ikicheza wakati Mbeligiji huyu huyu akiongoza ile timu ilikuwa ni balaa. Kwa hivyo nikiri bado Simba hatujapata wachezaji wenye uweledi sahihi wa kuipigania Simba kwa nguvu zao zote mfano wa Emanuel Okwi na baadhi ya wachezaji wengine kama matarajio ya wengi hasa ukichukulia huduma bora wanazozipata wachezaji wa Simba na unyonge na ziki unaowakabili wachezaji wa baadhi ya timu ambazo Simba inashindwa kupata ushindi. Tupo kwenye Dirisha dogo la usajili na usajili ni gharama tena sana lakini Simba wanalazimika kuingia sokoni kutafuta wachezaji tena haraka bila ya kuchelewa na si tu kufikiria mashindano ya klabu bingwa Africa bali kutetea ubingwa wake wa ligi kwanza kwani ukiangalia Azam walivyo fasta katika kukijenga kikosi chao unajua kabisa hawana utani na suala la ubingwa. Na si dhani kama kuna mchezaji au wachezji wa ndani wenye uwezo wa kukizi mahitaji ya Simba kwa hivi sasa.Mchezaji wa ndani akeshasajiliwa na Simba baada ya kuongeza bidii utashngaa anavyokuwa nyanya kwa hivyo wale waliokuwepo wazawa wanatosha kwa sasa. Lakini Simba kama tunataka kukata mzizi wa fitina kwa sasa katika kupata wachezaji wapiganaji basi itatubidi kuingia vitani kupata wachezaji hawa wawili Mbukinafaso wa Kotoko ya Ghana ambae ni mchezaji wao tegemeo na mwazoni mwa mwaka huu wamemsainisha mkataba wa miaka minne na ni moja ya silaha yao muhimu wakati kotoko wakijiandaa CAF confederation cup dhidi ya timu kutoka Cameroon. Huyu Mbukinafaso Sogne ni habari nyengine kabisa katika upambanaji wa kutafuta ushindi lakini kupatikana kwake si dhani kama kutakuwa rahisi na ndio maana nimetumia neno kuingia vitani katika usajili. Mchezaji mwengine Simba wakumuajiri kama uwezo upo basi lazima aletwe Fransisi kahata wa Gormahia tena bila ya kuchelewa kama Simba tuna ndoto ya kwenda kukabiliana na wababe wa Africa kwenye mashindano ya klabu bingwa na kuondoka na ushindi la sivyo tutakuja kumlaumu mzungu wa watu bure.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ufala bwana wachezaji rundo lote hilo we unaona hawafai tena

      Delete
  6. Mpira wa jana jamani acheni tu, kuna wakati nilikuwa natukana peke yangu baada ya kuwaona akina Boko, Kagele na Mohamed wakikosa magori ya kugusa. Binafsi sielewi ni kwanini, ila wazi jana kiungo tulizidiwa, kipindi cha kwanza beki ilikuwa haina mawasiliano mazuri, na pia kulikuwa hakuna muunganiko kati ya beki kwenda kwa viungo. Zaidi katika mpira ambao wamewahi kuucheza Simba msimu, mechi ambayo ilikuwa na makosa mengi ya beki na washambuliaji, ni hii ya jana. Kiukweli jana Simba mlinifanya nimfokee mwanangu bila sababu ya msingi. Kocha, kama huwa unasoma comments hizi, jana umekosa kabisa kujua nini ufanye baada ya mbinu zako za awali kukwama! Hatujaumbwa kushinda sisi Simba, ila kikosi tulichonacho hakistahili kufanya makosa ya mara kwa mara kama mchezo wa jana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic