November 23, 2018



Timu ya Simba na Lipuli leo zitakutana katika mchezo wa kwanza msimu huu baada ya msimu uliopita kocha Matola Selemani kupata sare na timu hiyo katika mechi zote mbili.

Mchezo wa leo utakuwa ni mgumu kwa timu zote na rekodi zinaonyesha kuwa wachezaji wote wa Lipuli FC walioifunga Simba walisajiliwa Simba.

Katika michezo hiyo waliyocheza uwanja wa Taifa, mfungaji wa Simba alikuwa ni Mwinyi Kazimoto kwa sasa anaichezea JKT Tanzania huku kwa Lipuli FC, Asante Kwasi yeye anaitumikia Simba.


Mchezo uliochezwa Samora, Lipuli FC walifunga kupitia Adam Salamba kwa sasa yupo Simba na lile la Simba lilifungwa na Laudit Mavugo ambaye mpaka sasa yupo Burudi akiwa ni mchezaji huru.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic