Uongozi wa timu ya Prisons ya Mbeya umesema kuwa upo katika hatua za mwisho kuweza kumpata kwa mkopo mshambuliaji wa Simba, Mohamed Rashid ili aweze kuongeza makali kwenye safu ya Ushambuliaji.
Rashidi alisajiliwa na Simba dirisha kubwa akitokea Prisons tangu kuondoka kwake wamekuwa wakipata taabu kupata matokeo, katika michezo 14 waliyocheza wameshinda 1 na kufunga mabao 7.
Kocha Mkuu, Mohammed Abdallah amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na uongozi wa Simba ili waweze kumpata mshambuliaji.
"Tupo kwenye mazunguzmo na Simba ili kuweza kumpata Mohamed Rashid kwa kuwa tatizo letu kubwa ni nafasi ya ushambuliaji," alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment