November 18, 2018


Ukiachana na kuelekea mechi ya kirafiki ambayo Yanga watakuwa wanacheza leo dhidi ya Namungo FC huko Ruangwa, timu hiyo ipo katika hatihati ya kuwakosa wachezaji wake wawili katika mechi zingine mbeleni.

Kikosi cha Yanga kitakachocheza leo kitakuwa hakina majina ya wachezaji Papy Tshishimbi na Juma mahadhi ambao bado hali zao hazijawa sawa kiafya.

Taarifa zinaeleza wachezaji hao wanasumbuliwa na majeraha jambo ambalo litawafanya wawe nje ya kikosi.

Yanga itapiga na Namnungo leo kwenye Uwanja wa Kasim Majaliwa huko Lindi na baada ya hapo kikosi kitaelekea mkoani Shinyanga kucheza na Mwadui FC ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara.

Kuelekea mechi hiyo mashabiki na wadau wengi wa Yanga wamekuwa na hofu juu ya kukosekana kwa wachezaji hao ambao wanaamini wanaweza kuisaidia timu kwa namna moja ama nyingine.


1 COMMENTS:

  1. Yanga hatuna hofu yoyote hao wachezaji 2 kutocheza na Namungo FC ya Lindi, kweli jamani ndio tuwe na hofu? Mbona mnatubeza sana jamani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic