YANGA YASHUSHA MASHINE TATU KALI MPYA
Yanga imempa ruhusa Kocha Mwinyi Zahera, kumalizana na mastaa watatu wa kigeni aliokuwa anawataka na wiki ijayo akisharudi Dar es Salaam watamfuata nyuma kuja kumwaga wino.
Spoti Xtra linajua Zahera ambaye sasa yuko kwenye timu ya taifa ya DR Congo akiwa kocha msaidizi amependekeza straika na kiungo Mkongo pamoja na winga Mghana ambao wote alishafanya nao mazungumzo ya awali akawa amekwama kutokana na fedha. Guylain Kisombe
Makuntima ndiye kiungo aliyekuwa akicheza Gabon na sasa karudi FC Lupopo ambaye Zahera anamtaka aje kuchukua namba ya Pappy Tshishimbi anayelalamikiwa na kocha huyo kwamba hafuati maelekezo na anacheza mpira wa shoo. Mbali na huyo pia winga anayemleta amekuwa akisisitiza
kwamba ni mwenye kasi na uwezo wa kupandisha mashambulizi na kutupia kwa maelezo kwamba Ibrahim Ajibu amekuwa akikosa mtu kama huyo.
Katika maelezo yake ya kiufundi amekuwa akililia straika mtupiaji zaidi ya Heritier Makambo ambaye amekuwa akimuangusha katika mechi za hivi karibuni.
Zahera ambaye familia yake inaishi Ufaransa, aliushukuru uongozi wa Yanga kwa kuafi kiana na mapendekezo yake na kumtaka afanye nao mawasiliano waje Dar haraka akishatua yeye.
“Natarajia siku chache baada ya kurudi Tanzania nitawapokea na mara moja kuanza nao maandalizi ya ligi na mambo mengine. “Yanga inapitia katika wakati mgumu sana jambo ambalo linawafanya hata wachezaji wangu
kujikuta wakipoteza morali, ila najua hili ni suala la muda tu siku si nyingi tutakuwa katika wakati mzuri hasa kama tutasajili wote hao niliowapendekeza kwenye dirisha hili dogo,” alisema Zahera.
Yanga angalau imeanza kupumua baada ya Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kukubali kurejea Jangwani ingawa bado mamlaka za soka zimesisitiza hazimtambui.
ww jichanganye kuona kuwa Tshishimbi hakufai, kuna wakati misimamo ni mizuri na muda mwingine ni hatari sana.
ReplyDeletehakuna kiungo anayejituma na mwenye idhamu kama huyo, ni viungo wawili tu kwa ligi ya tz, Mkude na huyo Tshishimbi, sasa muache aende azam akakutane na chirwa na ngoma, au atue simba akutane na mkude na okwi?kagere ndio utajua kuwa ligi ina ukatili, wewe ni kocha gani kila mchezaji hafuati maelekezo yako, mbona husemi kindoki uliyetuletea,kifupi hata makambo uliyemleta bado hatujaona makali yake, wachezaji uliowakuta ni wazuuri mbona husemi tambwe na kamsoko ambao wameshaanza kuchoka na ni haki yao kwa umri na matatizo waliyoyapata,.
Shortly ukiona kila mchezaji hakuelewi na ww ujue hueleweki hivyo tumia akili zaidi na ww usiwe mwandishi wa habari kila siku mtandaoni na wanahabari wenzako