December 28, 2018


KOCHA Mkuu wa timu ya Mbeya City, Ramadhani Nswanzurimo amepania kutibua rekodi ya wapinzani wao Yanga watakaocheza nao kesho katika mchezo wa Ligi Kuu uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mbeya City wana pointi 23 baada ya kucheza michezo 17 wakiwa wamepoteza michezo 6 na wameshinda michezo 5 huku sare wakitoa mara 5 wakiwa nafasi ya 7 watakutana na Yanga ambao mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Nswanzurimo amesema wamejipanga kiasi cha kutosha kupata pointi tatu hasa kutokana na kuwapa majukumu wachezaji wake kutafuta matokeo wakiwa uwanjani.

"Najua utakuwa mchezo mgumu kwetu ila hesabu zetu kubwa ni kupambana na kupata matokeo, hilo linawezekana kwa wachezaji kucheza kwa kujituma uwanjani," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Walisema wengi maneno hayo kuwa mtashinda dhidi ya yanga mwisho wa siku mnafungwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic