December 19, 2018




Uongozi wa Azam FC umesema kuwa unatambua ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi kushushwa kwao kileleni na Yanga hakuwapi hofu wanaamini watarejea kileleni.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema wana wachezaji bora na kikosi makini ambacho kinauwezo wa kubadilisha matokeo kwa namna kinavyopambana..

"Timu nyingi ambazo zinapambana nasi zinatambua upana wa kikosi chetu, hilo halina ubishi ni kutokana na usajili makini tuliofanya pamoja na mbinu bora za kocha wetu.

"Mtibwa Sugar wanafuata na tutacheza nao ugenini Morogoro, dawa ni moja tu kupata pointi tatu ili kuendelea kujiweka katika mazingira magumu hakuna kingine kitakachoturidisha kileleni zaidi ya ushindi," alisema.

Azam wamecheza michezo 16 hawajapoteza mchezo sawa na Yanga wamejikusanyia pointi 40 na kuachwa kwa pointi 4 na Yanga ambao wanashikilia usukani wakiwa na pointi 44 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic