Uongozi wa timu ya Halmashauri ya Kinondoni KMC umesema kuwa hawana hofu na kupambana na mabingwa watetezi, Simba hesabu zao ni kuchukua pointi tatu muhimu.
KMC imecheza michezo 16 ikiwa imefanikiwa kushinda michezo 4 na kupoteza michezo 3 na sare 9 imejikusanyia pointi 21 kibindoni itavaana leo na Simba uwanja wa Taifa.
Ofisa habari wa KMC, Anwar Binde amesema mipango ipo sawa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba wachezaji wamepewa maelekezo pamoja na mbinu za kuimaliza Simba.
"Wachezaji wanajua wajibu wao, wamepewa maelekezo maalumu na kocha mkuu, Ettiene Ndayiragije hakuna tatizo lolote tupo tayari kwa ajili ya mchezo hatuna hofu yoyote.
"Tumejiandaa kupata matokeo na morali kwa wachezaji ni kubwa hasa kwa ajili ya mchezo wetu tunajua tuna kazi kubwa kupata matokeo ila tupo tayari mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," alisema.
Kutoka Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment