BAADA YA KUMJIBU KOCHA WAKE, YANGA WAJA NA KAULI JUU YA HATMA YA KAKOLANYA NA KLABU
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema kuwa bado wanatambua kuwa kipa Beno Kakolanya kuwa ni mali yao.
Nyika amesema Kakolanya ni mali ya Yanga kwa kuwa bado ana mkataba na mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zikielezwa kuwa Kakolanya ameamua kujiweka kando Yanga kutokana na kutolipwa stahiki zake.
Uwepo wa taarifa hizo umeambatana na kuelezwa kuwa Wakala wa Kakolanya kufanya kazi katika klabu ya Simba, jambo ambalo wengi wanaamini anaweza akavunja mkataba na Yanga.
Hata hivyo Nyika ameeleza kuwa yote yanazungumzwa si ya kweli na akisisitiza kuwa mchezaji huyo ambaye alisajiliwa kutoka Tanzania Prisons haiadai chochote klabu kama ambavyo imekuwa ikitangazwa na kuandikwa.
Sasa mbona amegoma kucheza?
ReplyDeleteMbona hata Kocha Zahera amesema Kakolanya na wachezaji wengine wanaidai Yanga? Kudaiwa sio ajabu ila fanyeni jitihada kuwalipa haki zao wachezaji. Dunia hii nani hadaiwi ?
DeleteLkn swala la kujiuliza katika wachezaji wote wa yanga wanaoidai klab kama kweli inamaana yy kakolanya pekee yake ndiyo anayelijua deni? Maana sisikie wengine wanamigomo wanapiga mpira na timu inafanya vizuri tu sasa why kakolanya?
ReplyDelete