Uongozi wa timu ya Yanga umesema unaheshimu timu zote ambazo watacheza nazo kwenye mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup msimu huu ikiwa ni msimu wa nne.
Yanga watacheza na mshindi wa mchezo kati ya Ihefu FC na Tukuyu Stars mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa jumamosi, Mbeya.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wanatambua timu zote ni bora na zina uwezo wa kupata matokeo hivyo wanaamini mchezo wao utakuwa ni mgumu wanajipanga ili kupata matokeo.
"Hakuna timu ndogo, wote wana uwezo na tunawaheshimu hivyo mipango inaanza sasa kuweza kuwa imara, imani yetu tutapata matokeo ambayo tunayatarajia," alisema.
Msimu uliopita Yanga walikutana na Ihefu kwenye hatua ya awali ambapo walishinda kwa penati na mchezo wao dhidi ya Singida United waliocheza uwanja wa Namfua walitolewa kwa penati.
Wasipaki basi kama walivyozoea
ReplyDeleteKama wanapaki bus na wanashinda tatizo liko wapi ndugu?
Delete