December 13, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Ofisa Habari wake, Clifford Mario Ndimbo, limesema kuwa klabu ya African Lyon ilituma maombi ya mechi zake za nyumbani pale inapocheza dhidi ya Simba na Yanga zifanyikie Arusha.

Ndimbo amesema Lyon walituma barua wakiomba wafanyiwe mabadiliko ya Uwanja badala ya kuchezea Dar es Salaam na sasa iwe nje kwa kufanyika Arusha kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid.

Lyon ambao watakuwa na mechi dhidi ya Yanga Disemba 20 mwaka huu, watakipiga kwa mara ya kwanza na mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Bara baada ya maombi yao kufanikiwa.

Kutokana na mabadiliko hayo, Yanga sasa itawabidi kusafiri mpaka Arusha tayari kwa mtanange huo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga itakuwa inaenda kukipiga na Lyon wakiwa na juu ya kilele cha msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamejikusanyia alama 41 huku Azam ambao ni wa pili wakiwa na 40.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic