December 6, 2018


Nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco, amesema yupo tayari kucheza soka nje ya Tanzania endapo atapata nafasi hiyo, imeelezwa.

Bocco ambaye yupo na kikosi cha Simba Eswatin baada ya kumaliza kazi dhidi ya Mbabane Swallows, ameeleza kuwa endapo akipata nafasi hiyo hataweza kuipoteza kirahisi.

Nahodha Bocco ambaye hajawahi kucheza nje ya Tanzania, ameibuka na kauli hiyo baada ya kutupia mabao mawili katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Mbabane.

"Bado nina nafasi ya kucheza soka nje ya Simba na Tanzania, ninaamini nikipata nafasi nitaitumikia vizuri" alisema.

Wakati huo kikosi cha Simba kinatarajia kuwasili leo nchini baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 8-1 dhidi ya Mbabane.

5 COMMENTS:

  1. Boko ni mchezaji mzuri lakini sio mshambuliaji makini na nazungumza hili kwa upendo kabisa Kwamba Boko anawapotezea Simba idadi kubwa ya kubwa ya mabao ambayo angeweza kuyafunga kirahisi tu kama angelikuwa makini na mtulivu wakati anapopata nafasi za kufunga ambazo nyingi ni za wazi kabisa kwani kunako nafasi nne za wazi Boko anazozipata anaweza kufunga goli moja si dhani kama kiwango cha kuridhisha kwa foward namba moja na amabae ni kapteni wa timu.Ni hakika Boko anaweza kujirekebisha na kuwa yule Boko anaendana na juku la ukapteni kwani ana kila kitu anachohitajika kuwa nacho mchezaji hasa mshambuliaji ni umakini tu ndio unaomtesa.kwa hivyo kabla hajafikiria kuondoka simba basi ajirekebishe na suala ka umakini katika umaliziaji atatisha zaidi kwani kuna minong'ono ya wanasimba ya chini kwa chini kuwa wanatamani waongezewe mshambuliaji mmoja aliekuwa makini zaidi ya wale waliopo ndio roho zao zitatulia.

    ReplyDelete
  2. Kwel kabisa anapoteza nafas nyingi sana msimu huu tofauti na msmu jana au sjui tungur zmetawala

    ReplyDelete
  3. Boko umri umeshamtupa, wakati mwafaka wa kuondoka ligi ya bongo ilikuwa wakati ule alipopata nafasi SA, kwa sasa ategemee kuzeekea bongo kama akina Ngasa, Okwi nk.Kucheza nje kynahitaji jitahada na kujituma, sio lelemama.

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na suala kukosa umakini kwa Boko, tena sio tu katika nafasi nne anaweza kufunga moja, kumbuka mechi na Lipuli hapa Bongo, Boko alipata nafasi sita za kutulia na kufunga lakini kati ya hizo 6 hakufunga hata goli 1. Hivyo kiukweli kwa ushauri wa dhati kabisa, nampenda Boko kutokana na umbo lake kimpira, ana uwezo uwezo wa kutumia umbo lake kulifanya likawa silaha kwa beki, ana uwezo wa kuchekecha adui na pia ana kasi nzuri, lakini tatizo lake kubwa ni akiingia ndani ya 18 tu, cjui akili na fikra zake huwa zinahama ghafla na kurudi! yaani utashangaa maamuzi ya upigaji atakayoyafanya au hata kunyang'anywa mpira kirahisi au kupata kigugumizi cha miguu. Ajitathimini kwanza katika hilo, ili aweze kuwavutia mawakala wa timu za nje. Simba ni timu ambayo inathamini maendeleo binafsi ya wachezaji kutokana na vipaji vyao. Hivyo hawataweza kumzuia tena wanaweza kumpatia msaada zaidi katika kufanikisha lengo lake. Mwandishi pia unatakiwa kubalance heading na body. Unatuambia "Boko aamua kuitosa Simba", kaitosaje sasa! ni vitu tofauti na habari ya ndani. Ungetuambia tu kuwa "Boko aeleza ndoto zake za baadae" au "Boko aweka bayana kuhusiana na mpira wake nje ya Tanzania". Mnatuboa na huo UNAZI WENU.

    ReplyDelete
  5. woooote mmeongea vizuri sana, good advice!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic