December 24, 2018


Nahodha wa timu ya Simba, John Bocco amesema kuwa kocha Mkuu Patrick Aussems raia wa Ubelgiji aliwaambia wana uwezo wa kupata matokeo katika mchezo wa marudio wakiwa makini kutumia uwanja wa nyumbani dhidi ya Nkana FC ya Zambia.

Bocco aliwaongoza jana Simba kuweza kutinga hatua ya Makundi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Nkana FC ambayo mtanzania Hassan Kessy anaitumikia.

"Kocha alitupa mbinu kali na mpya za kutafuta matokeo hivyo tulichokifanya ni kufuata maelekzo na kujituma kutafuta matokeo na tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.

Mara ya mwisho Simba kufuzu hatua ya makundi ilikuwa ni msimu wa mwaka 2003 hivyo wamefanikiwa kufanya hivyo msimu huu ambapo kwa kufanikiwa kufuzu hatua hiyo watapewa zawadi ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambazo ndizo zilitumika kwenye usajili wa kikosi cha Simba msimu huu.

4 COMMENTS:

  1. Pale yanga wanapoizomea simba, badala ya Simba kushindwa kuwalipa wachezaji haki zao imekuwa imekuwa wachezaji wake wanapewa motisha wa 1.3 milioni shilingi badala ya kuondoka mikono mitupu. Amekuwa Imekuwa Simba ikiwapa wachezaji haki zao kabla ya kukauka jasho lao

    ReplyDelete
  2. Walikuwa wanakiponda kikosi cha bil moja...Mara ohh ya uturuki...Sasa bilion moja ikiyowekezwa kwenye timu italeta mabilioni mengine

    ReplyDelete
  3. Simba mdogo mdogo na hatimaye itakuwa katika level za TP Mazembe,Aly Ahli,Exparance etc wakati jirani zetu wanaendekeza kutembeza mabakuli

    ReplyDelete
  4. Boko aache kuongea aongeze uwezo uwanjani anakosa sana magoli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic