December 5, 2018


Kutokana na uwezi aliounesha kiungo fundi na mwenye balaa la aina yake, Clatous Chama katika mchezo wa jana dhidi ya Mbabane Swallows katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema mchezaji huyo anastahili kusajiliwa Barcelona.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameeleza kuwa Chama anastahili kuchukua namba ya Andres Iniesta ambaye ameshaondoka Catalunya ili kuchukua nafasi yake akiamini kuwa ni bora.

Aidha, Manara amemtaja kuwa Chama ndiye kiungo bora kuwahi kutokea katika soka la Tanzania huku akimsifia zaidi akiamini hakuna kama yeye kwa sasa.


6 COMMENTS:

  1. Kwa kweli kama wazambia ndivyo walivyo kama alivyo huyu Chama wa Simba basi lazima tuwaheshimu katika masuala ya mpira. Na sio tu kwamba anaujua mpira na kuufanya anavyopenda bali chama ni miongoni mwa wachezaji wapya kabisa pale simba lakini jinsi anavyopigana kwa ajili ya timu utazani amekulia Msimbazi,unamuona kabisa hana mchezo au masihara hata kidogo anapokuwa kazini.Na kama dhana ya kuleta wachezaji wa kigeni ili vijana wetu wajifunze kutoka kwa wageni basi huyu Chama mmoja anatosha kabisa kuwa shule kwa wale wenye nia ya kujifunza. Chama ana vitu vingi,ana madini ya aina nyingi kuanzia kichwani mpaka miguuni kiasi cha kujiuliza anafanya nini Tanzania? Ni mwanzo tu lakini Mungu akimuweka Chama mzima wa afya na salama basi watanzania tutashuhudia makubwa zaidi kutoka kwa mwamba wa Lusaka Triple C.

    ReplyDelete
  2. sifa nyingi sana !! tusubiri acheze na timu kubwa za Tunis na Misri !!

    ReplyDelete
  3. Hivi mnataka timu kubwa za namna gani? mbona tunapenda kubeza uwezo wa wachezaji na uwezo wa timu zao? Hivi unaweza kusema MBAMBANE SWALLOWS ni timu ndogo ile! Tusijidharau kiasi hicho, kila game lina plan yake lakini uwezo wa wachezaji unabaki pale-pale. Uwezo waliouonyesha Simba Nchi ya ugenini ni mkubwa sana, hata waarabu wanakaa chini, wakijitahidi wanatoa sare.

    ReplyDelete
    Replies
    1. binafsi siwezi kuwapa simba sifa nyingi kwa kuwatoa mbabane......atakapomtoa Nkana red devils ntakuwa na kila sababu ya kupongeza tena kwa nguvu.....kwakuwa natambua nkana red si timu ya kitoto.....hao mbabane hawaingii hata nusu kwa ubora wa nkana.

      Delete
  4. Timoth,Mbabane Swallows ni timu kubwa kuanzia lini?
    Kuwa karibu kikanda na hawa jamaa ndiko kulikokufanya ulizoee na kulisikia sana jina lao lakini hawana ukubwa wowote,seriously timu kubwa imeshiriki hatua ya makundi mara moja tu ndio mafanikio yao unaiita timu kubwa,hebu tuwe serious

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic