December 5, 2018


Na George Mganga

Baada ya kufanikiwa kuwaondoa Mbabane Swallows katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 8-1, Simba inaweza ikakutana na Nkana Red Devils ya Zambia ama UD Songo ya Msumbiji katika mchezo unaofuata.

Nkana ambayo mtanzania Hassan Kessy anaichezea itakuwa inavaana na Songo leo ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa mwanzo kumalizika kwa Songo kuchapwa mabao 2-1 wakiwa kwao.

Mechi ya leo itaamua kama Kessy anaweza akarejea Dar es Salaam kuja kukipiga na timu yake ya zamani endapo itamalizika kwa suluhu ama wakishinda.

Kuna uwezekano mkubwa kwa Nkana kushinda mechi hiyo kwani tayari wana faida ya bao moja la ugenini ingawa mpira una matokeo ya aina yake baada ya dakika 90 kumalizika.

Simba watacheza na mpinzani wake kati ya Nkana na Songo kati ya Disemba 15 au 16 na mechi ya marudiano itafanyika kati ya Disemba 27 na 28 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic