December 17, 2018





Unaweza kusema katika hali isiyotarajiwa, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, juzi Jumamosi alimtibua kocha wake, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji katika mchezo wao dhidi ya Nkana FC. 

Okwi, raia wa Uganda, alimtibua Mbelgiji huyo wakati alipotolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Shiza Kichuya. 

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Nkana jijini hapa, ulimalizika kwa Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1.

Wakati akitolewa uwanjani, Okwi alionekana kutofurahia uamuzi wa kocha wake huyo.

Baada ya kutolewa, hakusalimiana na mtu yeyote mpaka anaenda kukaa kwenye benchi na hata alipopewa bips avae kwa zaidi ya mara mbili, alikataa. 

Kutokana na hali hiyo, Aussems alisema: "Okwi hakuwa vizuri, niliamua kumtoa ili aingie mtu ambaye angeweza kuisaidia timu. 

"Tulikuwa tunahitaji ushindi, hivyo lazima ufanye vile kwa kumtoa mtu ambaye anaonekana hayupo mchezoni, lakini hilo alilofanya wala halinisumbui."

Ikumbukwe kuwa, baada ya mchezo huo wa juzi, timu hizo zinatarajiwa kurudiana wikiendi ijayo jijini Dar na mshindi wa jumla atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo na atakayetolewa anaenda kucheza 'play off' katika Kombe la Shirikisho Afrika.

1 COMMENTS:

  1. Kocha mweledi kwani kichuya alikkuja kuwasabishia balaa Nkana. Khassan kessy siku zote anasumbuka mbele ya Kichuya kila mtu na kiboko yake game inayokuja ingekuwa busara mmoja kati ya Okwi, Kagere au Boko kuanzia benchi wakamuanzisha kichuya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic