KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera tayari amejitengenezea jina kubwa kwamba yeye ni msema kweli pale kunapokuwa na kasoro ambayo yeye anaona inaweza kusemwa bila ya woga.
Watu kama Zahera wanaweza kuishi siku nyingi bila ya magonjwa kwa kuwa haweki vitu moyoni. Unapofika wakati wa kusema anafanya hivyo na mambo yanasonga mbele.
Hili ni jambo jema katika maisha ya mwanadamu yeyote kwa kuwa kuhifadhi vitu kama uliudhiwa, unatengeneza chuki ambayo uliyebaki nayo inaendelea kukuumiza muda wote.
Hivyo uamuzi wa Zahera unaweza kuwa ni sahihi zaidi kwa maana ya msema kweli, asiyeogopa na mwepesi wa kuchukua uamuzi ambao unafaa kuwa. Lakini kufanya uamuzi wake uwe bora zaidi, kuna mambo kadhaa ya kujifunza kwake na kwetu sisi.
Siku zinavyosonga kutakuwa na hukumu ambayo mwisho itatupa uhakika wa kwamba kweli Zahera alikuwa sahihi au la. Nitakuambia kwa nini.
Kocha Zahera ameonyesha kukerwa na uamuzi wa Kakolanya kugoma akidai maslahi yake. Lakini ninaamini hakupata nafasi ya kuzungumza naye na kujua huenda yeye aliahidiwa tofauti na viongozi kama ilivyo kwa wengine.
Mfano, kujua aliahidiwa mara ngapi, aliambiwa mara ngapi halikutekelezwa au alidanganywa mara ngapi. Mwisho ameamua kugoma na kero imekwenda kwa Zahera ambaye anaonyesha aliumizwa na kitendo hicho kwa kuwa alikuwa anamtegemea Kakolanya.
Kawaida, hata wewe ungekuwa kocha ungekerwa na uamuzi kama huo kwa kuwa katika kikosi unakuwa unamhitaji sana mtu kama Kakolanya. Wakati mwingine ungeweza kuwaza kama anakuangusha katika mipango yako.
Hii ni kawaida kabisa kwa sisi binadamu, hufikiria mipango yetu kwa maana ya kuwa wabinafsi bila kujali mipango ya wengine. Ukitaka kuwa mtenda haki, basi wakati mwingine vizuri pia kufikiria na raha na maumivu ya wengine.
Nilikuwa ninajiuliza, kama kweli Zahera ameweza kuuvuka ukuta wa Kakolanya kwa kulazimisha kuwa asirejee kikosini na kama atarudi basi yeye aondoke. Ni kweli hasa kwa kuwa tu ameamua hivyo kwa nia ya kuisaidia Yanga au kumsaidia Klaus Kindoki acheze.
Haya ni mawazo yangu ninayojaribu kuwaza kwa nguvu na usinilazimishe kufikiri kama wewe. Kwamba kwa kosa hilo na kama Kakolanya amemalizana na viongozi, ndio kweli aondoke Yanga.
Sasa Yanga imeingia gharama ya kusajili kipa mwingine. Je, fedha zilizotumika kumsajili, kwa nini Kakolanya asingelipwa fedha zake ili atulie na kuendelea kuitumikia Yanga?
Je, Kakolanya kawa tatizo kwa Kindoki ambaye mwanzoni, Zahera alitaka kutuonyesha ni bora zaidi ya Kakolanya. Au kubaki kwa Kakolanya kumezidi kumpa hofu Kindoki kwa kuwa watu wamekuwa wakihoji kubaki kwake na malipo yake makubwa wakati hana msaada.
Haya ni mawazo yangu, ninaendelea kuwaza tu na inawezekana katika uwazaji wangu ukawa sahihi au la. Lakini uhalisia wa mambo utajionyesha baada ya muda na kitu kizuri kwa Yanga ni mambo mawili, Zahera awe amepatia.
Nasema hivyo kwa kuwa baada ya ukuta wa Kakolanya, Zahera bado hajaumaliza ukata wa Yanga ambao ulimfanya hata Kelvin Yondani ambaye ni mkongwe na tunaijua kazi yake Jangwani lakini naye aligoma.
Maana yake, bado kuna wengine siku chache zijazo nao watachoka na ikiwezekana kugoma. Lakini kwa uoga wa msimamo wa Zahera wanaweza wasigome, lakini wakabaki na mgomo baridi ambao utamuathiri yeye kama kocha.
Ndio maana nilikuwa naona, mgomo wa wazi, unaoonekana na kusikika wazi kila sehemu, ulikuwa ni msaada kwa Zahera kwa kuwa angejua mwenye tatizo na likishughulikiwa, anarejea kazini akiwa safi. Lakini wale watakaogoma chinichini, watammaliza yeye.
Ishu ya Yanga ni PASUA KICHWA Yanga wana matatizo makubwa kuliko unavyodhani ndugu mwandishi. Jana Zahera alizungumza vizuri sana kuwa hakuzuia mchezaji kugoma. Alichosema aliwaambia wachezaji wachague moja kubaki nyumbani hadi walipwe au wavumilie waendelee kucheza huku wakiendelea kudai. ALichokataa yeye ni mchezaji mmoja mmoja kugoma kila siku kisha kumuharibia mipango yake. Tena alisema yapo makubaliano maalum baina yake na wachezaji. Kakolanya amekwenda tofauti na makubaliano hayo na ameonekana kumpuuza kocha kwani hata mgomo wake hakumwambia kocha. Bahati mbaya zaidi aliondoka usiku wa manane timu ikiwa kambini. Mazingira ya Kakolanya ni zaidi ya madeni yake kwa Yanga hasa ikizingatiwa Menaja wake ni kiongozi mwandamizi wa Simba na nafikiri tatizo liko hapo. Kumekuwa na hofu kuwa huenda akawa anatumiwa kuihujumu Yanga hasa ikizingatiwa Kakolanya ndio alikuwa kipa tegemeo hasa baada ya Kindoki kuboronga. Ishu ya Zahera kumgomea Kakolanya kurejea Yanga haihusiani na kumtengenezea mazingira Kindoki eti acheze. Kabwili anafanya vizuri Kindoki hatacheza mbele ya Kabwili labda apate majeraha.
ReplyDeleteBora hili andiko lingekuwa habari tofauti na hii habari ya kutuchanganya na hisia zisizo na mpango
DeleteBora hili andiko lingekuwa habari tofauti na hii habari ya kutuchanganya na hisia zisizo na mpango
DeleteUshauri wangu kwa muandishi ni kwamba usijaribu kutengeneza kitu kwa fikra zako tu ni bora ukaelewa kwa undani anacho/alicho kizungumza kocha wa Yanga sio ujaribu kutengeneza fikra ambazo hazipo una uweledi mzuri wa kuandika lakini katika hoja yako kama kocha anatengeneza mazingira ya kumtumia Kindoki hazina mantiki yeyote yeye ndio mpangaji wa timu kama kweli anataka kumtumia Kindoki nani atamzuia? Elewa malalamiko ya kocha sio upotoshe umma kwa kalamu yako na uandishi wako
ReplyDeleteMbona yeye Zahera alikuwa tayari kakusanya mabegi yake kurudi kwao Congo baada ya kudanganywa katika suala la usajili. Unajua sisi watanzania ni watu hovyo sana. Kitu gani hasa kinachoshinda kuindesha Yanga mpaka wanakuwa ombaomba? Hii nchi ina serikali inayosimamia maslahi ya wananchi wake kama yanga imeshindikana kujiendesha yenyewe kwa nguvu za wanachama wake, simple atafutwe muekezaji chini ya usimamizi wa serikali kwisha habari. Timu ya mpira sio mzigo ni biashara kwa watu wenye kujitambua sisi watanzania kila kitu tunangojea kufadhiliwa na sasa ndio unaona wazungu wanatuambia hakuna ufadhili mpaka turidhie wanaume kwa wanaume kurambana mavi? kiburi hicho wanakipata wapi cha kutulazimisha mambo kama hayo ya ajabu kama si kutuona ni watu wa hovyo tusioweza kujikizi wenyewe mpaka kwa misaada yao. Na Yanga nao kila kakukicha Manji we Manji we yaani ni kulilia mazingira ya kujizalilsha
ReplyDeleteManji sawa si tatizo lakini afuate misingi sahihi iliyowazi ya kuisadia Yanga kama taratibu zilizotumika Kwa watani wao Simba. Kuna ubaya gani Yanga kuiga kilichobora kutoka Simba? Mtawaachia wapiga madili wa mjini kuidhalilisha Yanga mpaka lini?
Kufikiria ni kufikiria tu. Kinachohitajika ni kuchanganua. Siku tulijua mpira unahitaji nidhamu tutaona hata timu yetu ya taifa ikipanda sawa na klabu zetu. Ama uchaguzi ni wetu kuwaheshimu wataalamu na kutambua wanajua tusichokijua ama kuendelea kupamba upuuzi wa wachezaji wetu magazetini
ReplyDeleteWanadai NI zaidi ya Wachezaji kumi, leo analipwa mchezaji mmoja ndani ya kamera nyingi na fedha zinaonyeshwa, je wakigoma wote wanaodai kwa hata kocha anadai hapo patakuwa na timu, zahera ni kocha mzuri na anaangalia jicho la tatu, TATIZO washabiki wengi wanaangalia waliposimama na sio wanapokwenda.
ReplyDelete