December 12, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema tayari umeshapata majina ya wachezaji wanne ambao itawatangaza kuwasili siku yoyote kuanzia leo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, amesema majina hayo ni siri huku akiwataka wanachama na wadau wa Yanga kuwa watulivu hivi sasa.

Nyika amesema tayari wapo kwenye mazungumzo mazuri na wachezaji hao ambapo amewataja baadhi yao kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Mwenyekiti huyo pia amezungumzia tetesi ambazo ni za moto hivi sasa kuhusiana na aliyewahi kuwa kiungo wa Simba, Haruna Moshi kuwa wapo kwenye mazungumzo naye kwa kukanisha uwepo wa taarifa hizo.

Nyika amefunguka kuwa hawana mazungumzo na Moshi japo akikiri kuwa ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu mkubwa katika mashindano ya ndani na hata nje ya nchi.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa rasmi Disemba 15 Jumamosi ya wiki ijayo ambapo TFF imezikumbuhsia timu kuhakikisha zinatumia mfumo wa TFF FIFA CONNECT.

9 COMMENTS:

  1. Yanga wamekuwa na kelele nyingi za usajili zisizo na mshiko wa maana. Tetesi katika masuala ya usajili ni lazima kokote kule Duniani lakini hizi za Yanga wanamuonesha nani wakati nguvu zao ni za kuungaunga na huku wachezaji waliowasajili msimu uliopita wanaendelea kugoma kwa kutolipwa pesa zao za usajili. Hao TFF au chama cha kutetea haki za wachezaji wako wapi? Wengi wa wachezaji wa Yanga wanadai haki zao za usajili mishahara hawajalipwa na wanaendelea kuteseka lakini huku viongozi wao wanasajili wachezaji wapya tena wa kigeni inamaana pesa wanazo lakini hawataki kulipa madeni kutoka kwa wachezaji hasa wazawa. Kwanini isiwepo sheria yakwamba kabla ya timu kusajili mchezaji mpya lazima imalizane na madeni ya zamani ya usajili kwanza maana wakati mwengine ni uonevu. Kakolanya hakugoma leo kutafuta haki zake lakini inaoneka hakuna msaada wowote anaoupata hata hao TTF hatujasikia kusema lolote kuhusu kakolanya. Yule ni mchzaji wa timu ya Taifa. Ni golikipa namba 2 wa timu ya Taifa na inaonekana amevunjika moyo na kuumizwa hadi kufikia kugoma na kuna hatari ya kupoteza kipaji chake. Vyombo habari navyo vinaungana na Zahera kocha wa Yanga kumkandamiza kakolanya wakati zahera yeye ndie mwenye kuleta wachezaji wapya na wachezaji hao hapana shaka wanakamilishiwa stahiki zao. Sasa tahadhari ichukuliwe kabla wachezaji wa Yanga hawajaingia kunako siasa za makundi kati ya wazawa na wageni. Kunako dhiki mara nyingi ni rahisi sana watu kuchukiana. Cha msingi si mgeni si mzawa lazima haki zao wote zihishikmwe na kuhakikisha kuwa wanalipwa madeni yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watakaosoma hoja hii basi ujumbe umewafikia.

      Delete
    2. sijaona point ya mana uloandika hapo......issue ya yanga na mipango yao waachie wenyewe.....wanajua wanachofanya ndo mana mpka sasa hawajafungwa na wanaongoza ligi.......ni ajabu wewe mishipa ya shingo inakusimama ktk kuikosoa yanga na madeni ya wachezaji wake wakati wahusika wenyewe hawajakatishwa tamaa na hilo ......wanaendelea kupambana uwanjani.....it means kwamba wanaelewa mazingira ambayo klabu na viongozi wao wanapitia kipindi hiki.

      Delete
  2. Masuala ya Yanga ni magumu kueleweka. Muhimu tunashinda mechi zetu na kuongoza ligi. Niwatakieni kila la kheri na wachezaji wetu.

    ReplyDelete
  3. SASA HAPA UNAZUNGUMZIA YANGA PICHA UNAWEKA YA SIMBA HII NINI?

    ReplyDelete
  4. Mbna habar zako nyngi in za uongo

    ReplyDelete
  5. Mbna habar zako nyngi in za uongo

    ReplyDelete
  6. Mtoto wa kiume unapoteza muda kuinanga Yanga kisa kudaiwa na wachezaji wake!! Ungetumia muda huo kutafuta hela ya kuitunza familia yako kaka... Au la bado unaishi kwa wazazi... Wanaodai wapo kimya wewe unahangaika nini? Tatizo kubwa mikia huwa mnategemea YANGA WAKIWA NA MIGOGORO NDIO MCHUKUE UBINGWA!! Timu ngapi zina malalamiko ya kiuchumi kibao!! Singida United wamekimbiwa na wachezaji wao upo kimya Ya Yanga yanakuhusu nini? Piga kimya wacha watu wasonge na shida zao... Watu wanapambana na hali zao wapotezee tu...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic