December 16, 2018


Na George Mganga

Wakati dirisha la usajili likifungwa saa 6 kamili usiku wa leo, kumekuwa na sintofahamu ya kipa namba moja wa Yanga, Beno Kakolanya kama ameachwa kikosini au ataendelea kubaki.

Sintofahamu hiyo inakuja kutokana na orodha ya wachezaji walioondolewa kwa mkopo kwenda timu zingine huku jina la Kakolanya likiwa halipo.

Yanga imewaondoa wachezaji wanne ambao ni Yusuph Mhilu, Pato Ngonyani, Said Mussa na Emmanuel Martin kwenda timu zingine kwa mkopo na ikiingiza wawili pekee ambao ni Haruna  Moshi na Ibrahim Hamid.

Kuhusu hatima ya kuachwa kwa Kakolanya inashindwa kujulikana kwa asilimia 100 kama amebaki baada ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kutangaza kutomuhitaji kipa huyo baada ya kugomea akidai kulipwa stahiki zake ikiwemo fedha za mshahara.

Zahera alimkataa Kakolanya na kuwaomba wanaompigania upatu wamtafutie timu nyingine ambayo wanaona itafaa yeye kwenda kucheza.

Kocha huyo ameonekana kukerwa na tabia ya Kokalanya ambaye alisajiliwa kutoka Tanzania Prisons kugomea mazoezi kisa akidai fedha.

Licha ya kukataliwa jina la Kakolanya halipo kwenye orodha ya wachezaji walioondolewa kwa mkopo ama kuachwa kabisa ingawa Zahera alisema hamtaki kikosini mwake.

Ukichana na kauli ya Zahera, Kakolanya mwenyewe amekuwa akisema yeye bado ni mchezaji wa Yanga na mpaka sasa ana mkataba na timu hiyo.

Kakolanya alisema licha ya maneno kutoka kwa Zahera haimaanini kuwa yeye si sehemu ya Yanga bali anatambua bado ni halali kuendelea kuitumikia timu ingawa anadai fedha zake ikiwemo za usajili na mshahara.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic