December 16, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umetaja rasmi majina ya wachezaji iliowatoa kwa mkopo kuelekea mahala pengine na wale iliowasajili kipindi cha dirisha dogo ambalo limefungwa leo saa 6 kamili usiku.

Yanga imewataja wachezaji Haruna Moshi kutoka African Lyon na Ibrahim Hamid kama mchezaji huru kuwa ndiyo waliosajiliwa ndani ya kikosi.

Aidha Yanga imewatoa kwa mkopo wachezaji Said Mussa na Pato Ngonyani kwenda African Lyon huku Yusuf Mhilu akienda Ndanda na Emmanuel Martin akienda Ruvu Shooting.

Baada ya kukamilisha usajili huo na kuwatoa kwa mkopo wachezaji tajwa hapo juu uongozi wa timu hiyo unawaomba wanachama na mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani leo.

Yanga imetoa ombi hilo wakati leo itakaposhuka dimbani kukipiga dhidi ya Ruvu Shooting ambapo mechi itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic