December 18, 2018


Mlinzi wa kulia wa Nkana ya Zambia, Mtanzania, Hassan Kessy, amewapiga biti wapinzani wao Simba kwamba wasifikirie kupata bao la ugenini kutawasaidia kwani wamejipanga vilivyo kushinda tena kwenye mechi ya ugenini.

Kessy juzi Jumamosi aliwaongoza Nkana kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Simba wakiwa nyumbani kwao Zambia katika mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kutokana na matokeo hayo, Simba wanahitaji ushindi wa bao 1-0 ili waweze kusonga mbele baada ya kupata bao la ugenini licha ya kufungwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa Championi Jumatatu, Kessy ambaye pia amewahi kuichezea Simba, amesema kwamba wapinzani wao wasijisahau baada ya kupata bao hilo la ugenini kwani wao lengo lao ni kuendeleza matokeo ya ushindi kama walivyopata wakiwa kwao.

“Simba wasione kwamba wamepata bao la ugenini ndiyo wakaona wamemaliza kila kitu, sisi tunataka kushinda mechi hiyo ya ugenini na ndiyo maana kwa sasa tumeshaingia kambini kujiwinda na mechi hiyo ya marudiano.

“Kwetu haya ni matokeo mazuri sana na tunataka tufanye muendelezo wake katika mechi ya pili, akili zetu ni kushinda mchezo huo na kusonga mbele, hivyo niwaambie Simba kwamba wasijisahau kabisa wakaona itakuwa kazi rahisi kwao,” alisema Kessy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic