WAZAMBIA WAKATA TAMAA CAF
Licha ya Nkana FC Jumamosi iliyopita kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, lakini mashabiki wa timu hiyo wameonekana kukata tamaa ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hali hiyo imekuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa kwanza wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Nkana uliopo hapa Kitwe, Zambia.
Muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mashabiki wa Nkana ambao ni raia wa Zambia, waliishiwa nguvu na kuonyesha sura za kukata tamaa wakiamini kwamba katika mechi ya marudiano hawataweza kuwaondoa Simba.
Ili Nkana ifuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo, inatakiwa kulinda ushindi wake huo katika mechi ya marudiano, wikiendi ijayo jijini Dar es Salaam.
Lakini kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Simba ikiwemo kupata bao moja ugenini, ndiyo inawafanya Wazambia hao kuamini kwamba licha ya kushinda, lakini hawawezi kuvuka.
Wapenzi na mashabiki wa Nkana wanaweza kukata tamaa lakini kwa Nkana ile tulioiona ikiifanya Simba pale kitwe kuwa timu ya kawaida sana sio timu ya kubeza na Simba wanatakiwa kujipanga haswa. Kwanza Simba wafahamu yakuwa ushindi ni ushindi na kama kisu basi Nkana ameshikilia mpini hivi sasa na ili kumpokonya basi Simba wanatakiwa kuwa na tahadhari zaidi la sivyo wataumia.
ReplyDeleteIkiwezekana Simba wanapaswa kuwa na kambi ya siri hasa uwanja wa kufanyia mazoezi kuelekea mechi na Nkana. Nkana hawakuwa wajinga kuanika wapi walikuwepo kuelekea ile mechi yao na Simba kule kitwe. Hawakuonekana mpaka suku ya mechi hata kwenye mechi conference na waandishi wa habari hawakupeleka kocha wao inaonekana jinsi gani walivyodhamiria kutinga hatua ya makundi. Simba na wachazaji wao waache kasumba yakuwa labda wanamchezaji mzambia na Nkana wanamchezaji mtanzania kutakuwa na upendo na undugu wakajilegezalegeza.Hakuna kabisa kitu kama hicho ,ubaya,ubaya tu. Katika mpira hakuna kitu kama hicho undugu na urafiki ni baada ya mechi. Hata kule ulaya wanapokutana kante na Pogba kati ya Chelsea na Man United moto unawaka wa kweli kweli lazima tujifunze kutokana na makosa.
ReplyDeleteUkiangalia Simba yetu haina mfumo mbadala wa uchezaji. Timu nyingi zinafeli kucheza na Simba kwa kuwa wanazidiwa udhoefu lakn si mbinu. Timu itakayoweza kuwa wabunifu zaidi ni rahisi kuifunga Simba. Mfumo wao wa 4 3 3 unakosa mantiki ndio maana Nkana waliweza kuwashika hasa kupitiliza kwa Nicolaus Gyan
ReplyDelete