December 6, 2018


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema bado ana kazi kubwa Jangwani. 

Ajibu ambaye ana mabao matano kwenye ligi, ametengeneza pasi tisa zilizozaa mabao ya timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye ni tegemo ndani ya kikosi cha Yanga ameeleza kuwa bado wana michezo mingi mbele hivyo wanahitaji kupambana villivyo ili kufanya vizuri.

“Kazi bado kwa kuwa kuna michezo mingi ambayo ipo mbele yetu. “Kila mchezaji hapa ana tabia yake na pia wengine hawakuwa kwenye ligi muda mrefu hivyo lazima tunashirikiana kufikia malengo,” alisema Ajibu.

Wakati Ajibu akifunguka hayo, Yanga hivi sasa wapo Sumbawanga ambapo wamepiga kambi ya muda mfupi kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Wakiwa mjini humo, mabingwa hao wa kihistoria jana walicheza mchezo wa kirafiki na Sumbawanga United ambayo walifungwa kwa mabao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic