December 23, 2018


Mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza kuwania kufunzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Nkana FC ya Zambia imemalizika kwa Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Dakika 5 za mwanzo Simba walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu.

Iliwalazimu Simba wasubiri mpaka dakika ya 29 akimalizia pasi ya Claytous Chama na dakika ya 45  Meddie Kagere aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya  James Kotei.

Kipindi cha pili dakika ya 88 Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga. 

Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3.

9 COMMENTS:

  1. Hawasimba ndo kilakitu kwangu kaka tuwaombeee

    ReplyDelete
  2. Mungu ibariki simba mungu ibariki taifa stars mungu ibariki TANZANIA.

    ReplyDelete
  3. Wekeni kichwa cha habari kama timu ya Tanzania imefanya kweli.Saleh Jembe hivi ingekuwa timu yenu mnayoifagilia ambayo ikifunga vibonde vya ligi...mnaandika kichwa cha habari eti imefanya maajabu..Alichofanya Sumba Leo ndio maajabu...!sio ule upuuzi mnaandikaga!

    ReplyDelete
  4. This is Simba
    this is Simba
    this is Simba

    ReplyDelete
  5. Wamebana wameachia. Mbwembwe zote kwishaaaaa. Hassan Kessy

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  6. Yanga walijitahidi sana kuwaharibia Simba lakini Mungu hakywa pamoja nao na hili ni fundisho kubwa sana

    ReplyDelete
  7. rudia kumhoji hassan kesy maana anapenda sana kuongea na kujifanya yeye ni kila kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic